Monday, November 3, 2014

Nyimbo Za Kikristo: 61-70

Nyimbo Za Kikristo 61. Bwana, Nami
I Have a Friend so Precious

1. Nimemwona rafiki Wa thamani kubwa,
Ana ni penda kwa 'pole, Kwa pendo amini:
Kuishi kutengwa naye, La, huku siwezi,
Tunakaa pamoja: Bwana nami.

2. Pengine ninachoka, Mimi mdhaifu,
Ndipo ninamtehemea, Alivyoalika;
Huniongoza njiani Pahali pa nuru
Twatembea pamoja Bwana nami.

3. Namweleza huzuni Nafuraha yangu,
Vile vinavyosumbua Vinavyopendeza;
Huniagiza kutenda Yanayonipasa
Twazungumza pamoja Bwana nami.

4. Ajua natamani Kuwavuta watu,
Hivyo ananipeleka Kutangaza neno;
Nitangaze pendo lake, Kwa nini akafa;
Twahubiri pamoja Bwana nami.

Nyimbo Za Kikristo 62. Napenda Kitabu Chake
I Love The Sacred Book Of God

1. Napenda kitabu chake, Kilichotoka mbinguni,
Barua kwangu ya Bwana Ujumbe wake wa upendo.

2. Humo ndani ya Kitabu Sura ya yesu naona
Karatasi zimekuwa, Wayo zake za Mwongozi.

3. Neno Lake ni maonju, Kubwe la asali tamu;
Natamani kuuonja Ule mkate wa uzima.

4. Mapenzi Yake Mwumbaji, Yanafunuliwa humo;
Hazina kuu ya hekima, Utajiri wa ajabu.

5. Mwangaza wa ulimwengu Angaza humo moyoni!
Uwe mwandamizi pote, Taa ya hatua zangu.


Nyimbo Za Kikristo 63. Niuonapo Msalaba
When I survey the Wondrous Cross

1. Niuonapo Msalaba,
Kristo aliponifia;
Kwangu pato ni hasara.
Kiburi nakichukia.

2. Na nisijivune, Bwana,
Ila kwa sadaka yako;
Upuzi sitake tena,
Zi chini ya damu yako.

3. Tangu kichwa hata nyayo,
Zamwangwa pendo na hamu.
Ndako pweke hamu hiyo.
Pendo zako zimetimu

4. Vitu vyote vya dunia,
Si sadaka ya kutosha;
Pendo zako zaniwia,
Nafsi, mali na maisha.


Nyimbo Za Kikristo 64. Piga Panda
Watchman Blow the Gospel Trumpet

1. Piga panda ya Injili, onyesha watu wote;
Ili anaye sikia Atubu aokoke.

Piga panda ya Injili, uipige kwa nguvu;
Mungu amekuagiza mateka wawe huru.

2. Uipige vilimani, kwa kila tambarare;
Pande zote, miji yote isikie Injili.

3. Uipige mipakani, barabarani pia;
Iwatangazie wote, wanakwitwa na Baba.

4. Uipige! Watu wengi wataka wawe huru;
Waanbie kwamba Yesu asema "Njoni Kwangu."

Nyimbo Za Kikristo 65. Twendeni Askari
Onward, Christean Soldiers!

1. Twendeni askari, watu wa Mungu; Yesu yuki mbele tumwandame juu
Ame tangulia Bwana vitani, Twende mbele kwani ndiye amini.

Twndeni askari watu wa Mungu
Yesu yuko mbele, tumwandame juu.

2. Jeshi la shetani, likisikia Jina la Mwokozi, litakimbia;
Kelele za shangwe zivume pote; Ndugu, inueni zenu sauti.

3. Kweli kundi dogo, watu wa Mungu, La mababa yetu ni letu fungu
Hatutengwi nao, moja imani tumaini moja, na moja dini.

4. Haya mbele watu nasi njiani, Inieni myoyo, nanyi sifuni;
Heshima na sifa yake mfalme, Juu hata chini sana zivume.


Nyimbo Za Kikristo 66. Roho Yangu Amka Sasa
Awake My Soul

1.Roho yangu amka sasa, mara jitahidi;
Shindano ni lake Bwana, Zawadi ni taji.

2.Sauti ni yake Mungu inayokuita;
Ndiyo alitekirimu taji ya uzima.

3.Mashahidi ndio wengi wanaokuoma;
Ya nyuma usifikiri bali mwendo kaza.

4.Bwana umetuanzisha katika shindano;
Kwa vile tunaposhinda ushindi ni wako.

Nyimbo Za Kikristo 67. Kesha Roho Yangu
Ny soul, be on Thy Guard

1. Kesha roho yangu, adui maelfu
Hujaribu Kuangusha, Kuvuta dhambini.

2. Ukeshe,uombe, ili usishindwe;
Fanya vita kila siku, omba msaada.

3. Kushinda ni bado: ulinde silaha;
Usiache kupigana hata una taji.




Nyimbo Za Kikristo 68. Tusimame Imara Mwambani
Firmly Stand For God

1. Umtetee Mungu duniani ijapo pepo kali zavuma;
Mwanbani pekee pana nguvu Dhambi ikilemea.

Tusimame imara katika mwamba,
Mwamba wa Kristo pekee;
Ndipo salameni tutasimama
Kule kitini pa enzi.

2. Itetee Haki kwa bidii, kwa moyo mnyofu wa imani;
Mwambani pekee Utashinda wingi wa upotevu.

3. Itetee kweli, itadumu, ijapokawia itashinda;
Mwambani pekee pana raha yaishapo tufani.

Nyimbo Za Kikristo 69. Cha Kutumaini Sina
My Hope is Built

1. Cha kutumaini sima ila damu yake Bwana,
Sina wema wa kutosha Dhambi zangu kuziosha.

Kwake yesu nasimama,
Ndiye Mwamba: ni salama;
Ndiye mwanba: ni salama;

2. Njia yangu iwe ndefu yeye hunipa wokovu;
Mawinbini yakinipoga nguvu zake ndio nanga.

3. Damu yake na sadaka nategemea daima,
Yote chini yakiisha mwokozi atanitosha.

4. Nikiitwa hukumuni, rohoni nina amani;
Nikivikwa haki yake sina hofu mbele zake.



Nyimbo Za Kikristo 70. Wapenzi Wa Bwana
Come, We that Love the Lord

1. Wapenzi wa Bwana ije raha yenu!
Imbeni nyimbo za raha, Imbeni nyimbo a raha:
Za ibada yenu. Za ibada yenu.
Twenenda zayuni, mji mzuri zayuni!
Twenenda juu zayuni,
Ni maskani ya Mungu.

2. Wasiimbe wao wasioamini,
Watoto Mungu ndio, watoto wa Mungu ndio
Waimbao chini, waimbao chini

3. Twaona rohoni baraka za Mungu
Tusijafika mbinguni, tusijafika mbinguni
Kwenye utukufu, kwenye utukufu.

4. Tutakapomwona masumbuko basi.
Huwa maji ya uzima. Huwa maji ya uzima.
Anasa halisi. Anasa halisi.

5 comments: