Monday, November 3, 2014

Nyimbo Za Kikristo: 91-100

91. Kaa Nami
Abide with Me

1. Kaa nami, ni isiku tena;
Isiniache gizani, Bwana.
Msaada wako haukomi;
Nili peke yangu, kaa nami.

2. Siku zetu hazakawi kwisha;
Sioni la kunifurahisha;
Hakuna ambacho kakikomi,
Isiye na mwisho kaa nami.

3. Nina haja nawe kila saa;
Sina mwingine wa kunifaa
Mimi nitaongozwa na nani
Ila wewe? Bwana, kaa nami.

4. Sichi neno uwapo karibu;
Nipatalo lote si taabu;
Kifo na kaburi haviumi;
Nitashinda kwako, kaa nami.

5. Nilalapo nikuone wewe,
Gizani mote nimulikiwe;
Nuru za mbinguni hazikomi,
Siku zangu zote; kaa nami.

92. Magharibi Jua
Day is Dyding in the West

1. Magharibi jua limekwisha kushuka,
Mwezi na nyota sasa vinamsifu Muumba wa usiku.

Mungu Mtukufu, Mungu Mkuu,
Wote juu mbinguni, na wanadamu chini Twakusifu.

2. Mpaji wa uhai, ukaaye mbinguni.
Utuhifadhi sisi, tufahamu gizani, U karibu.

3. Mapenzi yako makuu yawe nasi usiku,
Tuli usingizini, kucha vivyo roho Tushukuru.

4. Na utakapo kuja na nguvu kutawala,
Mungu wangu kubali kunichikua mimi Uliko juu.

Baba, Mwana, Roho, Mungu wetu,
Wote juu mbinguni, na wanadamu chini Twakusifu.

93. Jua La Rohoni Mwangu
Sun of My Soul

1. Jua la rohoni mwangu, mpendwa Mwokozi wangu;
Usiku giza hapana, ukiwa karibu Bwana.

2. Nikipata usingizi, nijaze fikara hizi,
Ni tamu sana, nilale pendoni mwako milele.

3. Kaa nami, ewe Bwana, Usiku kama mchana,
Nisiishi mbali nawe; ni uhai kuwa nawe.

4. Kama mtoto mnyonge ameshawisha atange,
Mtafute Ewe Bwana, ujirudishie tena.

5. Wagonjwa wape amani, waneemeshe maskini,
Walio, Mtulizi, wape wote usingizi.

6. Asubuhi tutokapo, tukaribishe tulipo;
Twingiapo duniani tuwe mwako mkononi.

94. Po Pote Mashamba Yajaa
Far And Near The Fields

1. Po pote mashamba yajaa, tele nafaka pevu,
Po pote yang'aa meupe bondeni na nyandani.

Mwenye mavuno, twasihi upeleke wavuni,
Wayakusanye mazao, hata kazi yaishe.

2. Wapeleke uchaoni, waende na jotoni,
Hata jua lishukapo wakusanye ko kote.

3. Enyi wakazi wa Bwana yaleteni mazao,
Na jioni ingieni kwake na furaha kuu.

95. Zileteni Zaka Kwa Hazina
Bring Ye All The Tithes

1. Sikieni neno la Mungu Wetu, Zileteni zaka kwa hazina
Leteni na mioyo yenu yote; mibaraka itakuja.

Zileteni zaka kwa hazina, kanijaribu sasa nazo;
Nitakupeni mibaraka, zaidi ya nafsi ya kupewa.

2. Wataka Roho Mtakatifu kwako? Uzilete zaka kwa hazina
Ukae karibu na Bwana wako, ndipo utakapo barikiwa.

3. Je! Unakasoro na Bwana wako? Uzilete zaka kwa hazina
Uzilete kama alivyosema, Ndipo utakapo barikiwa.

4. Ushukuru Bwana na moyo wote, unapoleta zaka ghalani;
Usadiki ahadi zake zote, ndipo utakapo barikiwa.

5. Tuimbe sote nyimbo za furaha, tunapoleta zaka ghalani
Twimbe kabisa na furaha kubwa, kwani tutabarikiwa.

96. Mali Yako Sasa
We Give Thee But Thine Own

1. Mali yako sasa, Bwana, tutatoa;
Hatuna yaliyo yetu, Yote ni vipaji.

2. Sisi watumishi, Twaungama deni;
Tunge irudisha kwake, Iliyo ya Bwana.

3. Utusaidie, Upendo kujua,
Kwa ajili yao wote Walio gizani.

4. Neno tumaini na kutegemea:
Kwamba lote tufanyalo, Tulifanye kwako.

97. Sioshwi Dhambi Zangu
What Can Wash Away My Sin?

1. Sioshwi dhambi zangu bila damu yake Yesu,
Hapendezewi Mungu bila damu yake Yesu.

Hakuna kabisa dawa ya makosa
Ya Kututukasa ila damu yake Yesu.

2. La kunisafi sina ila damu yake Yesu,
Wala udhuru tena ila damu yake Yesu.

3. Sipati patanishwa bila damu yake Yesu,
Hukumu yanitisha, bila damu yake Yesu.

4. Sipati tumaini bila damu yake Yesu,
Wema wala amani bila damu yake Yesu.

5. Yashinda ulimwengu, iyo damu yake Yesu,
Na kutufikisha juu, iyo, damu yake Yesu.

98. Nilikupa Wewe
I Gave My Life For Thee

1. Nilikupa wewe, damu ya moyoni,
Ili wokolewe, winuke ufuni.

Nimekunyima ni wewe? Umenipa nini?
Nimekunyima ni wewe? Umenipa nini?

2. Nilikupa myaka yangu duniani;
Upate inuka, kuishi mbinguni.

3. Nimekuletea, huku duniani;
Pendo na wokovu, zatoka mbinguni.

4. Nipe siku zako, Udumu mwangani;
Na taabu yako, wingie rahani.

Nafsi, nafsi, pendo, mali, twae Imanueli.
Nafsi, nafsi, pendo, mali, twae Imanueli.











99. Twende kwa yesu
Come To the Saviour, Make No Delay

1. Twende kwa Yesu mimi nawe, njia atuonya tuijue,
Imo chuoni; na mwenyewe, hapa asema njoo!

Na furaha tutaiona, myoyo iki takasa sana;
Kwako mwokozi, kuonana, na milele kukaa.

2. "Wana na waje," atwambia furahini kwa kusikia;
Ndiye Mwokozi wetu hasa, na tumtii, njoni.

3. Wangojeani? Leo yupo: sakiza sana asemapo;
Huruma zake zitwitapo, ewe kijana, njoo.

100. Kuwatafuta
Seeking The Lost

1. Kuwatafuta wasioweza, kuomba wamrejee Yesu,
Kuwaambia maneno yake "Njooni kwangu, nawapenda."

Nitakwenda (Nitakwenda) niwatafute wapotevu (Wapotevu) wageuke,
Waingie (Waingie) katika zizi la Mwokozi (la mwokozi) Yesu Kristo.

2. Kuwatafuta wasioweza, waonyeshwe Mwokozi wetu,
Kuwaongoza, wapate wote uzima ule milele.

3. Kazi hiyo nataka kufanya, leo nimesikia mwito
Kuwainua waangukao, waletwe kwake Yesu Njia.

1 comment: