Monday, November 3, 2014

Nyimbo Za Kikristo: 121-140

121. Katika Wenye Dhambi
Chief Of Sinners

1.Katika wenye dhambi Ndimi mkuu wao—
Ila yesu akaja, Kwa dhanbi alikufa,
Akamimina damu Niupate uzima.

2.Ajabu pendo lake! Pendo lililo kuu,
Pendo lisilo mwisho, Lidumulo milele—
Lililonitafuta Inawa sikupenda.

3.Ingawa ni mbaya Kristo ni vyote kwangu;
Ajua haja zangu; Huzuni zangu, zake;
Hata katika vita, Akiwapo salama.
122. Yote Namtolea Yesu
All to Jesus I Surrender

1.Yote namtolea Yesu, moyo wangu ni wake:
Ninavutwa na upendo, kwa hivyo, najitoa.

Yote kwa yesu, Yote kwa Yesu,
Upendo wako hushinda; Yesu, natoa.

2. Yote namtolea Yesu, Nainamia pake;
Nimeacha na anasa, kwako Yesu nipokee.

3. Yote namtolea Yesu, Nifanye niwe wako;
Nipe Roho yako, Bwana, anilinde daima.

4. Yote namtolea Yesu, nami naona sasa,
Furaha ya ukombozi, nasifu jina lake.
123. Yesu Kwa Imani
My Faith Looks up to Thee

1.Yesu kwa imani, nakutumaini, peke yako;
Nisikie sasa, na kunitakasa, ni wako kabisa
Tangu leo.

2. Nipe nguvu pia za kusaidia moyo wangu;
Ulikufa wewe, wokovu nipewe, nakupenda wewe,
Bwana wangu.

3.Hapa nazunguka katika mashaka, na matata;
Palipo na giza utaniongoza, hivi nitaweza
kufuata.
124. Umechoka Umesumbuka
Are You Weary?

1. Umechoka, je, umesumbuka? mwambie Yesu sumbuko lako;
Unayalilia yapitayo? mwambie Yesu pekee.

Mwambie Yesu sumbuko lako, yu rafiki amini,
Hakuna rafiki kama yeye, mwambie Yesu pekee.

2. Je, machozi yakulengalenga? mwambie Yesu sumbuko lako;
Walemewa na dhambi rohoni? mwambie Yesu pekee.

3. Waogopa shida na majonzi? mwambie Yesu sumbuko lako;
Wasumbukia mambo yajayo? mwambie Yesu pekee.

4. Kuanzia kifo kukutisha? mwambie Yesu sumbuko lako;
Watamania ufalme wake? mwambie Yesu pekee.



125. Uniangalie
There's Life In A Look

1. 'Uniangalie' atwambia Yesu aliyetufia;
Msalabani ni uzima, Hapa utaipata hazina.

Kutazama Kalwari, Kutazama Kalwari,
Ni kupewa kuishi Kuutazama mti.

2. Ninapojaribiwa ghafla, Shetani hatanitenga;
Nikitazama msalaba Nguzu nitaipata kwa Bwana.

3. Msalaba nitautazama Kila wakati, daima.
Ahadi nitategemea, Hovi kabisa sitaangukaa.

126. Nina Haja Nawe
I Need Thee Every Hour

1. Nina haja nawe kila saa;
Hawezi mwingine kunifaa.

Yesu nakuhitaji vivyo kila saa!
Niwezeshe Mwokozi, nkujia.

2. Nina haja nawe; kaa nami,
Na maonjo haya, hayaumi.

3. Nina haja nawe; kila hali,
Maisha ni bure, uli mbali.

4. Nina haja nawe, Nifundishe,
Na ahadi zako zifikishe.

5. Nina haja nawe; mweza yote,
Ni wako kabisa siku zote.

127. Nisalama Rohoni Mwangu
When Peace Like A River

1. Nionapo amni kama shwari, au nionapo shida;
Kwa hali zote umenijulisha ni salama rohoni mwangu.

Salama rohoni,
Ni salama rohoni mwangu.

2. Ingawa Shetani atanitesa, nitajipa moyo kwani,
Kristo ameona unyonge mwangu; amekufa kwa roho yangu.

3. Dhambi zangu zote, wala si nusu, huwekwa msalabani;
Wala sichukui laana yake, ni salama rohoni mwangu.

4. Ee Bwana himiza siku ya kuja, panda itakapolia:
Utakaposhuka sitaogopa ni salama rohoni mwangu.

128. Taamini Nitii Pia
When We Walk with the Lord

1. Namwandama Bwana kwa aliloneno,
Njia zangu huning'azia;
Na nikimridhisha atanirudisha,
Taamini nitii pia.

Kuamini, Njia pweke ni hii
Ya furaha kwa Yesu: Amini ukatii.

2. Giza sina kwangu wala hata wingu,
Yeye mara huviondoa;
Oga, wasiwasi, sononeko, basi;
Huamini nitii pia.

3. Masumbuko yote, sikitiko lote;
Kwa mapenzi hunilipia;
Baa, dhara, dhiki, vivyo hubariki.
Taanimi nitii pia.

4. Mimi sitajua raha sawasawa
Ila yote Yesu kumtoa:
Napata fadhili na radhi kamili,
Taamani nitii pia.

5. Nitamfurahia na kumtumaini,
Majumbani na njia-njia;
Agizo natenda; nikitumwa hwenda,
Huamini, nitii pia.

129. Kumtegemea Mwokozi
'Tis So Sweet To Trust

1. Kumtegemea Mwokozi, kwangu tamu kabisa;
Kukubali neno lake nina raha moyoni.

Yesu, Yesu namwamini, nimemwona thabiti;
Yesu, Yesu yu thamani, ahadi zake kweli.

2. Kumtegemea Mwokozi, kwangu tamu kabisa
Kuamini damu yake nimeoshwa kamili.

3. Kumtegemea Mwokozi, kwangu tamu kabisa;
Kwake daima napata, uzima na amani.

4. Nafurahi kwa sababu nimekutegema;
Yesu, M-pendwa, Rafiki, uwe nami dawamu.

130. Yesu Kwetu Ni Rafiki
What A Friend We Have In Jesus

1. Yesu kwetu ni rafiki, hwambiwa haja pia;
Tukiombawka Babaye, maombi asikia;
Lakini twajikosesha, twajitweka vibaya;
Kama tulimwomba Mungu, dua atasikia.

2. Una dhiki na maonjo? Unamashaka pia?
Haifai kufa moyo, dua atasikia.
Hakuna mwingine Mwema, wa kutuhurumia:
Atujua tu dhaifu: Maombi asikia.

3. Je, hunayo hata nguvu, Huwezi kwendelea,
Ujapodharauliwa. ujaporushwa pia.
Watu wange kudharau, wapendao dunia.
Hukwambata mikononi, dua atasikia.

131. Baba Anilinda
I Trust In God

1. Namtegemea Mungu niwapo
Humo barani na baharini,
Yeye wa mbinguni anilinda.
Baba wa mbinguni anilinda.

Namwamini, Mungu anitunza (anitunza)
Milimani (milimani) au baharini (baharini) Baharini
Moyo Wangu (moyo wangu.) aulinda (aulinda).
Baba wa mbinguni anilinda.

2. La waridi alinawirisha,
Na huyo tai juu angani,
Nami kweli ananilinda,
Baba wa mbinguni anilinda.

3. Tunduni mwa simba namwamini,
Kwenye vita ama gerezani,
Motoni na furikoni,
Baba wa mbinguni anilinda.

4. Bondeni mwa giza na upweke,
Mchunga wangu yuanilinda,
Kwa upole aniongoza.
Baba wa mbinguni anilinda.

131a. Kwa Mahitaji Ya Kesho
Lord for Tommorrow and It's Needs

1. Kwa mahitaji ya kesho, Sian ombi;
Unilinde nisitende Dhambi leo;
Nisiseme neno baya, Mkombozi,
Nisifikiri uovu, leo hivi.

2. Ningefanya kazi sawa Na kuomba;
Ningekuwa mtu mwema Kila saa;
Mapenzi yako nifanye, Na kutii;
Nitoe mwili dhabihu, Leo hivi.

3. kama keo ningekufa Kwa ghafula,
Nitegemee ahadi Zako Bwana.
Kwa mahitaji ya kesho sina ombi;
Uniongoze, Nishike Leo hivi.

132. Bwana Ni Mchunga
The Lord is My Sherpherd

1. Bwana ni Mchunga, Sitahiji;
Majani mabichi mlisho yangu.
Ananinywesha maji Matulivu;
Atanirudisha nikipotea.

2. Nipitapo bondeni mwa mauti
U mlinzi wangu—sitaogopa;
Fimbo lako latoshakunilinda;
Ukinifariji sina hasara.

3. Kati ya mateso mea waandaa,
Na kikombe changu kinafurika;
Umenipaka kichwani mafuta;
Nitaulizaje zaidi kwako?

4. Wema na fadhili zinifuate
Siku zangu zote hata milele;
Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana
Katika ufalme wa pendo lake.




133. Po Pote Na Yesu
Anywhere With Jesus

1. Po Pote na Yesu nina furaha; Anitumako Yesu ndiyo raha.
Asipokuwako hapanifai, Akiwapo Yesu, mimi sitishwi.

Po pote, po pote, sina mashaka:
Po pote na Yesu naweza kwenda.

2. Akiwapo yesu, si peke yangu; Na nijapotupwa, akali wangu;
Ajaponiongoza njia nbaya, Niwapo na Yesu nashukuria.

3. Akiwapo yesu naweza lala, naweza pumzika hata kiyama;
Kisha nitakwenda kwake milele, akiwapo Yesu furaha tele.
134. Tafuta Daima Utakatifu
Take Time to be Holy

1. Tafuta daima utakatifu;
Fanya urafiki na wakristo tu;
Nena siku zote na Bwana wako,
Baraka uombe kwa kila jambo.

2. Tafuta saima utakatifu:
Uwe peke yako ukimwabudu;
Ukimwangalia Mwokozi wako,
Utabadilishwa kama alivyo.

3. Tafuta daima utakatifu;
Kiongozi wako awe Yesu tu;
Katika furaha au huzuni
Dumu kumfuata Yesu Mwokozi.

4. Tafuta daima utakatifu;
Umtawaze Roho moyoni mwako,
Akikuongoza katika haki,
Hufanywa tayari kwa kazi yake.



135. Kwa Maombi Nachangamka
Sweet Hour Of Prayer

1. Saa heri ya maombi, sasa kwako tunarudi,
Sumbuku ya kuondoa, shida zitu na pungufu.
Taabuni mara nyingi, roho zetu zimepona,
Mashakani tumeshinda, wakati wa saa tamu.

2. Saa heri ya maombi, Twapelika dhiki zetu
Kwake aliyeahidi kubariki wenye haja.
Huagiza tumwendee, tutegemee neno lake,
Hivyo tumwekee yote, wakati wa saa tamu.

3. Saa heri ya maombi, tutazidi kuingia
Bomani mwetu na ngome, hata tuishapo mwendo.
Yesu atatusikea, tutamtafuta daima,
Na tutakapolutana tutamwona—saa tamu!


136. Niwe Kama Yesu
Teach Me Father

1. Unifundishe, Baba; Ile njia ya sala;
Uniendeshe sana, Niwe kama Yesu.

Niwe kama Yesu, Niwe kama Yesu,
Uniongoze, Baba; Niwe kama Yesu.

2. Unipe pendo, Baba, Watu kuwaokoa;
Nyumbani na mjini. Niwe kama Yesu.

3. Na unifahamishe, Wakati ndio mfupi;
Unibidishe, bwana, Niwe kama Yesu.
137. Saa Heri Ya Sala
'Tis the Blessed Hour of Prayer

1. Saa heri ya sala tunapojidhili,
Kama tukija kwake yesu rafiki.
Tukiwa na imani kwamba yu mlinzi,
Waliochoka sana watapata raha.

Saa ya sala, iliyo heri;
Waliochoka sana watapata raha.

2. Saa heri ya sala, ajapo mwokozi,
Ili awasikie watoto wake.
Hutwambia tuweke miguuni pake
Mizigo yetu yote: tutapata raha.

3. Saa heri ya sala, wawezapo kuja
Kwa Bwana Yesu wanaojaribiwa;
Moyo wake mpole, atawarehemu;
Waliochoka sana watapata raha.

4. Saa heri ya sala tutakapopewa
Mibaraka ya roho, tukimwamini;
Kwa kuamini kweli hatutaogopa;
Waliochoka sana watapata raha.

138. Nitakuandama Kote
I Will Follow Thee

1. Nitakuandama kote, nitakapoagizwa,
Wewe ukiniongoza nami nitaandama.

Nitakuandama Kote, naam, ulinifia;
Kwa neema yako Bwana napenda kuandama.

2. Njia ijapoparuza kwa miiba na fujo,
Ulitangulia Mbele nami nitaandama.

3. Nijapokuta taabu na majaribu kote,
Nakumbuka shida yako, nami nitaandama.

4. Nijapoona ukiwa na mateso makali,
Wewe uliyatikiza nami nitaandama.

5. ijapo wanipeleka vilindini mwa giza,
Wewe uliyatikiza nami nitaandana.

139. Uliniimbie Tena
Sing them over again

1. Uliniimbie tena, Neno la uzima;
Uzuri wake nione, Neno la uzima;
Neno hili zuri, lafundisha kweli:

Maneno ya uzima ni maneno mazuri,
Manemo ya uzima ni naneno mazuri.

2. Kristo anatupa sote, Neno la uzima:
Mwenye dhambi asikie Neno la uzima:
Latolewa bure, Tupate wokovu:

3. Neno tamu la Injili, neno la uzima;
Mwenye dhambi asikie Neno la uzima:
Litatutakasa, kwa haki ya Mwana:

140. Hivi Nilivyo Unitwae
Just as I am

1. Nitwae hivi nilivyo, umemwaga damu yako,
Nawe ulinyoniita, Bwana Yesu, sasa naja.

2. Hivi nilinyo; si langu kujiosha roho yangu;
Nisamehe dhambi zangu, Bwana Yesu, sasa naja.

3. Hivi nilivyo; sioni kamwe furaha moyoni,
Daima ni mashakani, Bwana Yesu, sasa naja.

4. Hivi nilivyo kipofu, maskini na mpungufu;
Wewe ndiwe u tajiri, Bwana Yesu, sasa naja.

5. Hivi nilivyo, mimi tu, siwezi kujiokoa;
Na wewe hutanikataa, Bwana Yesu, sasa naja.

6. Hivi nilivyo; mapenzi yamenipa njia wazi;
Hali na mali sisazi, Bwana Yesu, sasa naja.

No comments:

Post a Comment