Monday, November 3, 2014

Nyimbo Za Kikristo: 81-90

81. Siku Sita Zimepita
Another Six Days' Work

1. Siku sita zime pita, Sabato tena karudi;
Shangilie roho yangu, itukuze kwa busara.

2. Msifuni awapaye pumziko tamu wachovu,
Kwake roho yatulizwa, kupita siku nyingine.

3. Moyo wetu ufurahi, na kutoa mashukuru;
Ujalizwe raha ile, yasipitikwa kamwe.

4. Raha hiyo ya rohoni, ni amana ya pumziko
Ambalo limewekwa juu, kikomo cha masumbuko.

82. Ni Siku Ya Furaha
O Day Of Rest

1. Ni siku ya furaha, ni siku ya nuru;
Nasi twaona raha, Kuja kushukuru;
Leo watu wa Mungu, wadogo, wakubwa,
Hukaribia mbingu, lilipo baraka.

2. Leo, ndiyo bandari, nasi twawasili,
Hiyo bustani nzuri, ya nyingi fadhili:
Kijito cha baridi kimefanya ziwa,
Na kiu ikizidi, twanywa maridhawa.

3. Leo ngazi na iwe ifakayo juu,
Mawazo na yasiwe ya duniani tu;
Leo ni kujilisha chakula cha mbingu,
Na kujifurahisha kwa mambo ya Mungu.

83. Ewe Skuli Ya Sabato
Sweet Sabbath School

1. Ewe skuli ya Sabato,
U pazuri sana;
Moyo wangu wanivuta,
Nije kwako leo.

Sabato . . . ni nzuri . . .
Sabato . . . ni nzuri . . .
Moyo wangu wanivuta,
Nije kwako leo.

2. Moyo wangu mpotovu,
Hapa una raha;
Ndipo nimwonapo Yesu,
Nije kwako leo.

3. Hapa Yesu mwenye pendo
Aniita pole:
Nimtolee moyo Yeye,
Nije kwako leo.

84. Ikumbuke Sabato
Don't Forget the Sabbath

1. Ikumbuke kote Sabato ya Bwana,
Siku tamu na bora, kupita nyingine;
Yatuletea raha, na furaha kweli,
Mwanga wake hungaza, urembo wa Yesu.

Karibie, karibie, Sabato tamu;
Karibie, Yesu pia, Bwana wa raha.

2. Itakase kweli, ukamsifu leo,
Yeye aliye sema "Mimi ndiye njia";
Nasi tukimfuata mkombozi hapa.
Atatunywesha tele maji ya uzima.

3. Siku ya nderemo! Tupishe wakati,
Tukimwimbia Yesu Rafiki Mpendwa;
Mponya wetu leo, U mwema ajabu!
Ukae kwetu, Bwana, moyoni daima.

85. Salama Tumepita
Safely Through Another Week

1. Salama tumepita, safarini juma hii,
Tumwendee Mwokozi, atubariki sasa:
Siku hiyo ya raha, siku bora ya juma;
Siku hiyo ya raha, siku bora ya juma.

2. Utupe nuru leo toka hazina yako;
Ondoa dhambi zetu, tupokee na pendo;
Mikono yapumzika, tuishi ndani yako,
Mikono yapumzika, tuishi ndani yako.

3. Twakusanyika hapa, tusifu jina lako;
Ukaribie kwetu, tupe neema Bwana;
Utamu tusikize, wa raha ya milele:
Utamu tusikize, wa raha ya milele:

4. Injili yako leo, ishike wenye dhambi;
Itupe nguvu nyingi, iponye wenye shida;
Mioyo yetu shangaza, vyakula utulishe,
Mioyo yetu shangaza, vyakula utulishe.

86. Ukaribie Tena
Welcome, Welcome, Day of Rest

1. Ukaribie tena, ewe siku ya raha;
Roho yakusalimu kama mwanga wa mbingu.

2. Raha yako tulivu, yafurahisha moyo;
Yatuliza taabu, hata waisha mwendo.

3. Ee siku takatifu, sifa na maombi,
Na kutuhekimisha., baraka yako kubwa.

87. Siku Ya Sabato
Thy Holy Sabbath Lord

1. Siku ya Sabato, siku takatifu,
Watu wako Mungu wetu, waipenda sana.

2. Ulitakasa, uliibariki,
Siku hiyo ya Sabato, siku yako Bwana.

3. Nasi tubariki tukikuabudu,
Katika siku ya raha, siku yako Bwana.

4. Halafu mbinguni, pamoja na Wewe.
Tunataka kuzishika Sabato za Bwana.

88. Siku Hii Ya Sabato
How Sweet Upon This Sacred Day

1. Siku hii ya Sabato, Tamu kufikiri
Juu ya Mungu na Mbingu Kuacha dunia.

2. Tamu kusikia Neno Toka mhubiri
Anayefundisha toba, Tupate uzima.

3. Katika vita na dhambi, Ikiwa twashindwa,
Yeye atatupa nguvu Aonaye moyo.



















89. Asubuhi
Lord, In The Morning

1. Bwana asubuhi kucha nitakuinua
Sauti yangu kuomba, nipate baraka.

2. Nakuomba roho yako niongozwe nayo;
Nifanye yanipasayo, na mapenzi yako.

3. Wanaokutegemea, U Mlinzi wao;
Matumaini wanayo, utayatimiza.

4. Na kwa wingi wa fadhili, Nyumbani mwako juu
Nitaingia na wimbo, Pale kusujudu.

90. Mapya Ni Mapenzi
New Every Morning

1. Mapya ni mapenzi hayo, Asubuhi tuonayo;
Saa za giza hulindwa, Kwa uzima kuamka.

2. Kila saku, mapya pia, Rehema, wema na afya,
Wokovu na msamaha, Mawazo mema, furaha.

3. Tukijitahidi leo Na mwendo utupasao,
Mungu atatueleza Yatakayompendeza.

4. Mamboyetu ya dunia Bwana atayang'aria,
Matata atageuza Yawe kwetu ya baraka.

5. Yaliyo madogo, haya Bwana tukimfanyia,
Yatosha: tutafaidi Huvuta kwake zaidi.

6. Ewe Bwana, siku zote, Tusaidie kwa yote:
Mwendo wetu wote vivyo, Uwe kama tuombavyo.

2 comments: