Saturday, November 24, 2012

Nyimbo Za Kikristo 51 - 60

Nyimbo Za Kikristo No. 51: Kuwa Na Yesu

 

1.      Yesu Mwokozi, kwa hakika, Hunipa furaha na amani;
Mrithi wa wokovu wake, Natakaswa kwa damu yake.

 

Habari hiyo wimbo wangu, Daima nitamsifu Yesu.
Habari hiyo wimbo wangu, Daima nitamsifu Yesu.

 

2.      Nijitoapo nina raha, Na kwa imani namwona Bwana;

Aniletea malaika, Wananilinda, niokoke.

 

3.      Hali na mali anaitwaa, Katika Yesu nabarikiwa;
Nikimngoja kwa subira, Wema wake unanitosha.

 

Nyimbo Za Kikristo No. 52: Nipe Biblia

 

1.      Nipe Biblia nyota ya furaha, wapate nuru wasafirio;
Hakuna la kuzuia amani,
Kwani Yesu alituokua.

 

Nipe Biblia neno takatifu,
Nuru yake itaniongoza;
Sheria na ahadi na upendo,

Hata mwisho vitaendelea.

 

2.      Nipe Biblia nihuzunikapo ikinijaza moyoni dhambi;
Nipe neno zuri la Bwana Yesu,
Nimwone Yesu Mwokozi wangu.

 

3.      Nipe Biblia nipate kuona, hatari zilizo duniani;
Nuru ya neno lake Bwana Yesu,
itaangaza njia ya kweli.

 

4.      Nipe Biblia taa ya maisha; Mfariji tunapofiliwa;
Unionyeshe taa ya mbinguni,
Nione utukufu wa Bwana.

 

Nyimbo Za Kikristo No. 53: Napenda Kuhubiri!

 

1.      Napenda kuhubiri habari ya Yesu,
Ya Bwana wa fahari na pendo zake kuu.
Huhubiri napenda kwa hali na mali;
Mwenyewe Nimeonja najua ni kweli.


Napenda kuhubiri kisa cha Bwana Yesu,
Ya Bwana wa fahari na pendo Zake Kuu.

 

2.      Napenda kuhubiri mambo ya ajabu
Na tukiyatafikiri yapita Dhahabu.
Kuhubiri napenda ya yaliyonifaa;
Nami sana napenda hayo kukwambia.

 

3.      Napenda kuhubiri, hunifurahisha
Tamu yake habari haiwezi kwisha.
Napenda kuhubiri wa gizani nao;
hawana muhubiri wa kweleza chuo.

 

4.      Kuhubiri napenda hata wajuao;
Kusikia hupenda kama wenzi wao.
Nako kwenye fahari nikiimba wimbo
Nitaimba habari ya Mwokozi huyo!

 

Nyimbo Za Kikristo No. 54: Nataka Nimjue Yesu!

 

1.      Nataka nimjue Yesu, na nizidi kumfahamu,
Nijue pendo lake tu, wokovu wake kamili.

 

Zaidi zaidi, nimfahamu Yesu,
Nijue upendo wake, wokovu wake kamili.

 

2.      Nataka nimjue Yesu, na nizidi kusikia

Anenapo kitabuni, kunidhihirisha kwangu.

 

3.      Nataka tena zaidi, daima kupambanua
Mapenzi yake, nifanye yale yanayompendeza.

 

4.      Nataka nikae, kwa mazungumzo matamu.
Nizidi kuwaonyesha wengine wokovu wake!

 

Nyimbo Za Kikristo No. 55: Twapanda Mapema

 

1.      Twapanda mapema, na mchana kutwa

Mbegu za fadhili hata jioni,

Twangojea sasa siku za kuvuna;

Tutashangilia wenye mavuno.

 

Wenye mavuno, wenye mavuno,

Tutashangilia wenye mavuno.

Wenye mavuno, wenye mavuno,

Tutashangilia wenye mavuno.

 

2.      Twapanda mwangani na kwenye kivuli;

Tushindwe na baridi na pepo;

Punde itakwisha kazi yetu hapa:

Tutashangilia wenye mavuno.

 

3.      Twapanda kwa Bwana mbegu kila siku.

Tujapoona taabu na huzuni;

Tuishapo shinda atatupokea:

Tutashangilia wenye mavuno.

 

Nyimbo Za Kikristo No. 56: Waponyeni Watu

 

1.      Walio kifoni, nenda waponye.

Uwatoe walio shimoni;

Wanaoanguka uwainue;

Habari njema uwajulishe.

 

Walio kifoni waokoeni,

Mwokozi yuko huwangojea.

 

2.      Wajapokawia anangojea,

Awasubiri waje tobani;

Mwokozi hawezi kuwadharau,

Huwasamehe tangu zamani.

 

3.      Na ndani ya moyo wa wanadamu

Hawamo shida, tena huzuni;

Lakini kwa Yesu huna rehema

Kuwaponya na kuwaokoa.

 

4.      Walio kifoni, nenda waponye

Kazi ni yetu, zawadi iko;

Nguvu kuhubiri Bwana hutoa

Kwa subira tuwavute sasa.

 

Nyimbo Za Kikristo No. 57: Usikatae Kazi

 

1.      Usikatae Kazi yake Bwana; Ukae tayari Kuifanya kazi;

Uende po pote Mungu akwitapo, Nawe utaona Furaha kazini.

 

Njoo, We! Usiikatae; Njoo, We! Uifanye kazi;

Usiikatae Kazi yake Bwana, Ili hatimaye usikatazwe juu.

 

2.      Usiikatae Kazi yake Bwana; Kwa nini kawia? Fanya kazi leo.

Mavuno meupe, Wachache Wavuni, Onyesha furaha Kwa kazi ya Bwana.

 

3.      Usiikatae Kazi yake Bwana, Kukataa pendo Kwako ni Hatari.

Saa ya rehema, Yesu akiomba, Ziungame dhambi, Zifutwe mbinguni.

 

Nyimbo Za Kikristo No. 58: Zitakuwa Nyota Tajini?

 

1.      Leo ninafikiri ya nchi nzuri Ninayotaka kuiona;

Nisimamapo karibu na Mwokozi, Tajini zitakuwa nyota?

 

Sijui tajini mwangu kama nyota

Zitang'aa kila wakati!

Nitakapoamka katika majumba,

Zitakuwa nyota tajini?

 

2.      Kwa nguvu za Bwana nitafanya kazi, Nitavuta roho za watu,

Ili niwe na nyota katika taji, Bwana anapotupa tunu.

 

3.      Nitakuwa na furaha nikimwona, Kuweka miguuni pake

Watu waliovutwa kwa ajili ya Kazi yangu na Roho yake.

 

Nyimbo Za Kikristo No. 59: Fanyeni Kazi Zenu

 

1.      Fanyeni kazi zenu, usiku si mbali;

Kesheni saa zenu vumilieni:

Kwa Yesu tumikeni na hiyo Injili.

Sana wahubirini watu wa mbali.

 

2.      Fanyeni kazi zenu giza yasongea;

Na wengi wenzi wenu wamo gizani.

Msipoteze moja dakika ni hizi;

Mwana atarejea mwisho wa kazi.

 

3.      Fanyeni kazi zenu, hivi jua lachwa;

Wote walio kwenu apenda Mungu:

Na sisi tumjuaye na tuwafundishe,

Ili Yesu ajaye tumfurahishe.

 

Nyimbo Za Kikristo No. 60: Nitakwenda Utakaponituma

 

1.      Pengine sio milimani Utakaponiita;

Pengine siyo baharini wala palipo vita;

Lakini, nitajibu, na njia siijui.

Bwana, nitajibu, ni tayari Kwenda uniagizapo.

 

Ukiwa pamoja nami, Bwana, Mlimani, baharini,

Niende utakaponiita; Na fuata uendeko.

 

2.      Pengine leo kuna neno, Neno tamu la pendo,

Ambalo Yesu anataka Ninene kwa upole;

Ukiwa pamoja nami, Bwana, Nitamtafuta leo

Yule aliyepotea mbali: Nitasema upendavyo.

 

3.      Pahali pako bila shaka Pa kuvuna shambani,

Kazi niwezayo kufanya Kwa Yesu Mkombozi;

Hivi nikikutegemea, Kwa kuwa wanipenda,

Mapenzi yako nitafanya, Na niwe upendanyo.

Thursday, November 8, 2012

Nyimbo Za Kikristo No. 21 - 30

Nyimbo Za Kikristo No. 21: Baba Twakujia
 
1.Bwana twakujia, Uwe msaada;
Uwe kimbilio, twakusihi.
Dunia ni giza tukitengwa nawe;
Tufariji hapa, baba yetu.
 
Baba teakujia, tu dhaifu, usitugeue, tusikie.
 
2.Salama tulinde, kati ya taabu;
Uwe raha yetu mashakani.
Roho yasumbuka, Baba tujalie;
Twakuomba sana, tupe nguvu.
 
3.Neema utupe, tukubali kwako;
Moyo wetulinda, safarini;
Tuongoe mbele, tupate kushinda
Na kufika ng'ambo, kule kwako.
 
Nyimbo Za Kikristo No. 22: Usinipite
 
1.Usinipite, Mwokozi, unisikie;
Unapozuru wengine, usinipite.
 
Bwana, Bwana unisikie;
Unapozuru wengini, usinipite.
 
2.Kiti chako cha rehema, nakitazama;
Magoti napiga pale, nisamehewe.
 
3.Sina ya kutegemea, ila wewe tu;
Uso wako uwe kwangu: nakuabudu.
 
4.Wewe tu u Mfariji: sina mbinguni,
Wala duniani pote, Bwana mwingine.
 
Nyimbo Za Kikristo No. 23: Yesu Furaha Ya Moyo
 
1.Yesu, furaha ya moyo! Hazina ya pendo, na nuru.
Yote yatupendezayo, yasilinganishe nawe.
 
2.Kweli yako ya daima, wawajibu wakwitao,
Ni siku zote u mwema kwao wakutafutao,.
 
3.U mkate wa Uzima, kupokea ni baraka,
Twanya kwako u kisima roho zikiburudika.
 
4.Mwokozi twakutamani, kwako roho hutulia;
Twakushika kwa imani, nawe watubarikia.
 
5.Yesu, ndiwe kwetu mwanga, tufurahishe daima;
Giza ya dhambi fukuza, uwe mwanga wa Uzima.
 
Nyimbo Za Kikristo No. 24: Jina La Yesu Tamu
 
1.Jina lake Yesu tamu Tukilisikia,
Hutupoza, tena hamu Hutuondolea.
 
2.Roho ilioumia Kwalo hutibika,
Chakula, njaani pia; Raha, tukichoka.
 
3.Jina hili ni msingi, Ngao, ngome, mwamba,
Kwa hili napata ungi, Kwangu ni akiba.
 
4.Yesu, Mchunga, Rafiki, Mwalimu, Kuhani,
Mwanzo, mwisho, na amina, mali yangu yote!
 
5.Moyo wangu hauwezi Kukusifu kweli;
Ila sifa zangu hizi, Bwana, zikubali.
 
Nyimbo Za Kikristo No. 25: Taji Mvikeni
 
1.Taji mvikeni. Taji nyingi sana,
Kondoo mwake Kitini, Bwana wa mabwana;
Nami tamsifu Alikufa kwangu,
Ni Mfalme mtukufu, Seyidi wa mbingu.
 
2.Taji mvikeni Mwana wa Bikira;
Anazovaa kichani Aliteka nyara;
Shilo wa manabii Mchunga wa watu
Shina na tanzu ya Yesu wa Bethliehemu.
 
3.Taji mvikeni Bwana wa Mapenzi;
Jeraha zake ni shani Ni vito nya enzi,
Mbingu haina Hata malaika
Awezae kuziona pasipo kushangaa!
 
4.Taji mvikeni Bwana wa Salama;
Kote - kote duniani Vita vitakoma;
Nayo enzi yake itaendelea,
Chini ya miguu yake, Maua humea.
 
Nyimbo Za Kikristo No. 26: Tutokapo Tubariki
 
1.Tutokapo tubariki, Utupe kufurahi;
Tuwe na upendo wako, Neema ya kushinda.
Nawe utuburudishe tukisafiri chini.
 
2.Twatoa sifa, shukrani Kwa neno la injili;
Matunda yake wokovu Yaonekane kwetu;
Daima tuwe amini Kwa kweli yako, Bwana.
 
3.Siku zetu zikizidi Tuzitoe kwa Yesu;
Tuwe na nguvu moyoni Tusichoke njiani;
Hata tutakapoona Utukufu wa Bwana.
 
Nyimbo Za Kikristo No. 26a: Tupe Amani
 
1.Mungu mtukufu Aliyeumba pepo kuvuma Na radi kali;
Toa neema unapotawala, Tupe amani Bwana wa wema.
 
2.Mungu wa neema, Nchi imeacha Amri tukufu Na Neno lako;
Hasira zako Zisituharibu, Tupe amani, Bwana wa wema.
 
3.Mwumbaji wa haki, Watu wabaya Wamedharau Utukufu wako;
Lakini wema wako Utadumu; Endesha kweli Bwana wa wema.
 
4.Tunakutolea Ibada safi Kwa ajili ya Wokovu wako;
Hivi tunaziimba Sifa zako; Wako uwezo Na utukufu.
 
Nyimbo Za Kikristo No. 27: Tena, Mwokozi, Twalitukuza Jina Lako
 
1.Tena, Mwokozi, twalitukuza
Jina lako lenye kupendeza,
Twangojea neno la amani,
Kabla hatujakwenda nyumbani.
 
2.Tupe amani njiani mwetu,
Wewe u mwanzo, u mwisho wetu;
Dhambini kamwe isiingie
Midomo ikitajayo wewe.
 
3.Utupe amani usiku huu,
Ili gizani kuwe nuru kuu.
Tulinde kwa kuwa kwako Bwana.
Usiku ni sawa na mchana.
 
4.Tupe amani ulimwenguni
Ndiyo dawa yetu majonzini;
Na ikitwita sauti yako,
Tupe amani milele kwako.
 
Nyimbo Za Kikristo No. 28: Jina La Thamani
 
1.Jina lake Yesu tamu, Lihifadhi moyoni;
Litatufariji ndugu, Enda nalo po pote.
 
Jina la (Thamani) thamani, (thamani)
Tumai la dunia
Jina la (Jina la thamani-tamu!) thamani,
Furaha ya mbinguni.
 
2.Jina la Yesu lafaa Kama ngao vitani,
Majaribu yakisonga, Omba kwa jina hili.
 
3.Jina hili la thamani Linatufurahisha,
Anapotukaribisha, Na tunapomwimbia.
 
4.Mwisho wa safari yetu Tutakapomsujudu,
Jina hili tutasifu Furaha ya mbinguni.
 
Nyimbo Za Kikristo No. 29: Yesu, Nakupenda
 
1.Yesu nakupenda, U mali yangu,
Anasa za dhambi sitaki kwangu;
Na mwokozi aliyeniokoa
Sasa nakupenda, kuzidi pia.
 
2.Moyo umejaa mapenzi tele
Kwa vile ulivyonipenda mbele,
Uhai wako ukanitolea
Sasa nakupenda, kuzidi pia.
 
3.Ulipoangikwa Msalabani
Tusamehewe tulio ndambini;
Taji ya miiba uliyoivaa,
Sasa nakupenda, kuzidi pia.
 
4.Mawanda mazuri na masikani
Niyatazamapo huko mbinguni,
'Tusema na taji nitakayovaa
Sasa nakupenda, kuzidi pia.
 
Nyimbo Za Kikristo No. 30: Yesu, Unipendaye
 
1.Yesu unipendaye kwako nakimbilia,
Ni wewe utoshaye mwovu akinijia.
Yafiche ubavuni mwako maisha yangu;
Nifishe bandarini, wokoe moyo wangu.
 
2.Ngome nyingine sina; nategemea kwako,
Usinitupe Bwana, nipe neema yako,
Ninakuamania, mwenye kuniwezesha;
Shari wanikingia, vitani wanitosha.
 
3.Nakutaka Mpaji, vyote napata kwako;
Niwapo muhitaji, utanijazi vyako;
Nao waangukao wanyonge wape nguvu;
Poza wauguao, uongoze vipofu.
 
4.Mwana umeniosha moyo kwa damu yako;
Neema ya kutosha yapatikana kwako;
Kwako Bwana naona kisima cha uzima;
Mwangu moyoni, Bwana, bubujika daima.
 
  --   http://www.fastmail.fm - A no graphics, no pop-ups email service  

Nyimbo Za Kikristo No. 40 - 50

Nyimbo Za Kikristo No. 41: Roho Mtakatifu
1. Roho Mtakatifu, Kiongozi amini;
Utushike mkono Tulio wasafiri;
Utupe kusikia Sauti ya upole;
"Msafiri fuata, Naongoza nyumbani."
2. Wewe ndiwe rafiki, Msaada karibu;
Tusiache shakani; na tukiwa gizani
Utupe kasikia Sauti ya upole;
"Msafiri, fuata, Naongoza nyumbani."

3. Siku zetu za kazi, Zikiwa zimekwisha,
Wala hatuna tamaa Ila mbingu na sala;
Utupe kusikia Sauti ya upole;
"Msafiri fuata, Naongoza nyumbani.

Nyimbo Za Kikristo No. 42: Ewe Roho wa mbinguni

1. Ewe roho wa mbinguni, Maombi sikia!
Makao yako yafanye Mioyoni mwetu.

2. Kama nuru, tupenyeze, Giza uondoe;
Siri yako tuone, Na amani yako.

3. Kama moto, tusafishe, Choma dhambi yetu;
Roho zetu ziwe zote Hekalu la Bwana.

4. Kama umande, na uje, Utuburudishe,
Moyo 'kavu utakuwa Ni wenye baraka.

5. Kaka upepo Ee Roho, Katika Pentekoste
Ukombozi Utangaze, Kwa kila taife.

Nyimbo Za Kikristo No. 43: Furaha Gani!

1. Furaha gani na ushiriki,
Nikimtegemea Yesu tu!
Baraka gani, tena amani,
Nikimtegemea Yesu tu!
Tegemea, salama bila hatari;
Tegemea, tegemea Mwokozi Yesu.
2. Nitaiweza njia nyembamba,
Nikimtegemea Yesu tu;
Njia 'tazidi kuwa rahisi,
Nkimtegemea Yesu tu!

3. Sina sababu ya kuogopa,
Nikimtegemea Yesu tu;
Atakuwa karibu daima,
Nikimtegemea Yesu tu.

Nyimbo Za Kikristo No. 44: Urafiki Wa Yesu

1. Hakuna rafiki kama Yesu, Hakuna, hakuna!
Tabibu mwingine wa rohoni, Hakuna hakuna!
Yesu ajua shida zetu; Daima ataongoza.
Hakuna rafiki kama Yesu, Hakuna, Hakuna!
2. Wakati ambapo hapo yeye, Hapana, hapana!
Wala giza kukutenga naye, Hakuna, hakuna!

3. Aliyesahauliwa naye, Hakuna, hakuna!
Mkosaji asiyempenda, Hakuna, hakuna!

4. Kipawa kama mwokozi wetu, Hakuna, hakuna!
Ambaye atanyimwa wokovu Hakuna, hakuna!

Nyimbo Za Kikristo No. 45: Mwanga Umo Mwoyoni.

1. Mlimani pana mwanga, Mwanga wa jua zuri
Shambani na baharini Jua tukufu liko;
Mwanga ulio mkubwa Umo moyoni mwangu,
Kwa kuwa Yesu alipo Hapa pana mwangaza.
Mwangaza ulio mzuri, Mwanga umo moyoni;
Akiwapo Bwana Yesu Pana mwanga moyoni.
2. Kama mavazi kukuu Ninavua huzuni:
Nguo nzuri za furaha Umenipa za kuvaa.
Nakuandama rohoni Hata nyuba ya juu
Iliyopambwa vizuri Katika pendo lako.

3. Ulinikomboa Yesu; Maisha yangu, mali,
Vyote ni nyako, Mwokozi—Daima nikusifu.
Nakuandama rohoni Hata nyumba ya juu
Iliyopambwa vizuri Katika pendo lako.

Nyimbo Za Kikristo No. 46: Miguuni Pake Yesu

1. Miguuni pake Yesu, Maneno yake tamu;
Pahali palipo heri, Niwepo kila siku,
Miguuni pake Yesu Nakumbuka Upendo
Na hisani vyake kwangu, Vimenivuta moyo.

2. Miguuni pake Yesu, Hapa pahali bora
Pakuweka dhambi zangu: Pahali pa pumziko.
Miguuni pake Yesu, Hapa nafanya sala,
Kwake napewa uwezo, Faraja na neema.

3. Unibariki Mwokozi, Ni miguuni pako,
Unitazame kwa pendo, Nione uso wako.
Nipe Bwana nia yake Ili ionekane
Nimekaa na Mwokozi Aliye haki yangu.

Nyimbo Za Kikristo No. 47. Ni Heri Kifungo

1. Ni heri kifungo kinachotufunga
Mioyo yetu kwa pendo la Kikristo.

2. M-bele ya Baba Tunatoa sala,
Hofu, nia masumbufu Yetu ni mamoja.

3. Tunavishiriki Matata na shida,
Na mara nyingi twatoa Chozi la fanaka.

4. Tunapoachana Moyoni twalia;
Lakini tutakutana M-wisho mbinguni.

Nyimbo Za Kikristo No. 48: Ninakupenda Zaidi

1. Ninakupenda zaidi, Ya vyote vingine;
Kwani umenipa raha, Na amani, Bwana.
Nusu haijatangazwa (Tangazwa)
Ya upendo wako;
Nusu haijatangazwa (Tangazwa)
Damu hutakasa (takasa).
2. Nakujua u karibu Kuliko dunia;
Kukukumbuka ni tamu kupita kuimba.

3. Kweli wanifurahisha, na nitafurahi;
Pasipo upendo wako naona huzuni.

4. Itakuwaje Mwokozi, Kukaa na wewe,
Ikiwa ulimwenguni Tuna furaha hii?

Nyimbo Za Kikristo No. 49: Ninaye Rafiki

1. Ninaye rafiki naye Alinipenda mbele;
Kwa kamba za pendo lake Nemefungwa milele:
Aukaza moyo wangu, Uache ugeuzi,
Ninakaa ndani yake, Yeye kwangu milele.

2. Ninaye Rafiki ndiye Aliyenifilia;
Alimwaga damu yake kwa watu wote pia;
Sina kitu mimi tena, Nikiwa navyo tele;
Pia vyote ni amana Ndimi wake milele.

3. Ninaye Rafiki naye Uwezo amepewa;
Atanilinda mwenyewe, Juu 'tachukuliwa;
Nikitazama mbinguni Hupata nguvu tele;
Sasa natumika chini, Kisha juu milele.

4. Ninaye Rafiki naye Yuna na moyo mwema,
Ni Mwalimu Kiongozi, Mlinzi wa daima;
Ni nani wa kunitenga, Na mpenzi wa mbele?
Kwake nimetia nanga, Ndimi wake milele.

Nyimbo Za Kikristo No. 50: Mungu Nawe Nanyi Daima

1. Mungu nawe nanyi daima; hata twonane ya pili,
Awachunge kwa fadhili, Mungu nawe nanyi daima.
Hata twonane juu, hata twonane tena kwake;
Hata twonane juu, Mungu nawe nanyi daima.
2. Mungu nawe nanyi daima. Mungu nawe nanyi daima,
Awafunike mabawa. Awalishe, awakuze;

3. Mungu nawe nanyi daima. Mungu nawe nanyi daima,
Kila wakati wa shida Awalinde hifadhini:

4. Mungu nawe nanyi daima. Mungu nawe nanyi daima,
Awabariki na pendo Ambalo halina mwisho; Mungu nawe nanyi daima.

Nyimbo Za Kikristo No. 30 - 40

Nyimbo Za Kikristo No. 31: Niimbe Pendo Lako
1. Niimbe (niimbe) pendo lake,
Pendo la (pendo la) Yesu Bwana;
Sababu (sababu) alitika
Kwa Baba akafa.
Niimbe (niimbe) pendo lake;
Sifa kuu (sifa kuu) nitatoa;
Akafa (akafa) niwe hai, --
Niimbe pendo lake.
2. Machozi (machozi) alitoa
Ijapo (ijapo) sijalia;
Maombi (maombi) yangu bado,
Aniombeapo.
3. Upendo (upendo) kubwa huo!
Dunia (dunia) haijui
Samaha (samaha) kwa makosa
Kubwa kama yangu.

4. Hapana (hapana) tendo jema
Ambalo (ambalo) nilitenda,
Nataka (nataka) toka leo
Nimwonyeshe pendo.

Nyimbo Za Kikristo No. 32: Tangu Kuamini

1. Ninao wimbo mzuri, Tangu kuamini;
Wa Mkombozo Mfalme, Tangu kuamini.
Tangu kuamini, Jina lake 'tasifu,
Tangu kuamini, Nitalisifu jina lake.
2. Kristo anatosha kweli, Tangu kuamini,
Mapenzi yake napenda, Tangu kuamini.

3. Ninalo shuhuda sawa, Tangu kuamini,
Linalofukuza shaka, Tangu kuamini.

4. Ninalo kao tayari, Tangu kuamini,
Nililorithi kwa Yesu, Tangu kuamini.

Nyimbo Za Kikristo No. 33: Karibu Sana

1. Karibu sana univute, Karibu sana daima nawe.
Bwana napenda unishike, Unilinde nisianguke nawe.
Unilinde nisitengwe nawe.

2. Karibu sana, sina kitu sina, Sadaka kwa Bwana Yesu,
Isipokuwa moyo wangu: Uutakase katika damu,
Uutakase katika damu.

3. Karibu sana, Wewe nami. Ninafirahi kuacha dhambi-
Anasa zote na kiburi: Nipe Yesu niliyemsulibi,
Nipe Yesu niliyemsulibi.

4. Karibu sana, hata mwisho. Hata mbinguni nisimamapo:
Daima dawamu niwepo Nitakapoona usi wako,
Nitakapoona uso wako.

Nyimbo Za Kikristo No. 34: Hadithi Kisa Cha Yesu

1. Nipe habari za Yesu, Kwangu ni tamu sana:
Kisa chake cha thamani Hunipendeza sana.
Jinsi malaika wengi walivyo imba sifa,
Alopoleta amani kwa watu wa dunia.
Nipe habari za Yesu, Kaza moyoni mwangu;
Kisa chake cha thamani Hunipendeza sana.
2. Kisa cha alivyogungwa Peke yake jangwani.
Jinsi alivyomshinda Jaribu la Shetani;
Kazi aliyoifanya, Na siku za huzuni,
Jinsi walivyomtesa: Yote ni ya ajabu!

3. Habari za Msalaba Alivyosulubiwa;
Jinsi walivyo mzika, Akashida kaburi.
Kisa chake cha rehema. Upendo wake kwangu.
Alivyotoa maisha Nipokee wokovu.

Nyimbo Za Kikristo No. 35: Nimekombolewa Na Yesu

1. Nimekombolewa na Yesu na sasa nimefurahi;
Kwa bei ya mauti yake mimi ni mtoto wake.
Kombolewa! Nakombolewa na damu.
Kombolewa! Mimi mwana wake kweli.
2. Kukombolewa nafurahi, Kupita lugha kutamka;
Kulionyesha pendo lake, mimi ni mtoto wake.

3. Nitamwona mfalme wangu katika uzuri wake,
Ambaye najifurahisha katika torati yake.

4. Najua taji imewekwa mbinguni tayari kwangu,
Muda kitambo atakuja ili alipo niwepo.

Nyimbo Za Kikristo No. 36: Siku Kuu

1. Ni siku kuu siku ile ya kumkiri Mwokozi!
Moyo umejaa tele kunyamaza hauwezi.
Siku kuu! Siku kuu! Ya kwushwa dhambi zangu kuu!
Hukesha na kuomba tu, ananiongoza miguu.
Siku kuu! Siku kuu! Ya kwoshwa dhambi zangu kuu!
2. Tumekwisha kupatana, mimi bwake, yeye mbwangu,
Na sasa nitamwandama, nikiri neno la Mungu.

3. Moyo tulia kwa Bwana, kiimi cha raha yako;
Huna njia mbili tena: uwe naye, yote ndako.

Nyimbo Za Kikristo No. 37: Pendo Lako, Ee Mwikozi

1. Pendo lako, Ee Mwokozi, Hushinda pendo zote!
Kaa nasi, ndani yetu, Furaha ya mbinguni.
Yesu u rehema tupu, Safi na Kusamehe,
Mfariji mwenye huzuni Ziondoe machozi.

2. Roho yako ya upendo, Tuma kwa kundi lako;
Hebu tuirithi raha, Iliyoahidiwa,
Uondoe moyo mbaya, U Mwanzo tena Mwisho;
Timiza imani yetu, Ili tuwekwe 'huru.

3. Yesu, uje kwetu sasa, Tupokee huruma;
Rudi kwetu, tena kamwe Usituache pekee,
Tungekutukuza leo, Pamoja na malaika,
Imba na kutoa sifa, Ingia kwa ibada.

4. Sasa, Bwana, kazi yako, Imalize moyoni;
Takasa hekalu lako, Wokovu kamilisha!
Safisha viumbe nyako Katika wakati huu;
Tupumzike 'toka dhambi, Tuingie mbinguni.

Nyimbo Za Kikristo No. 38: Nasifu Shani Ya Mungu

1. Nasifu dhani ya Mungu, mweneza bahari,
Muumba pia wa mbingu, jua, nyota, mwezi.
Ni tukufu yako shani, mtengeza mambo
Ya nyakati na zamani, yasiyo na mwisho.

2. Kadiri ya nionayo, yakusifu Mungu;
Nchi niikanyagayo, na hayo mawingu;
Hakuna hata unyasi, usiokukuza;
Na upepo wavumisha, au kutuliza.

3. Nami kwa mkono wako, naongozwa sawa,
Ni pato nikusipo, kukwomba ni dawa;
Umenizingira nyuma, na mbele baraka,
Maarifa ya ajabu! Yanishinda mimi!

Nyimbo Za Kikristo No. 39: Ati, Kuna Mvua Njema

1. Ati, kuna mvua njema yanya yenye neema;
Watu wanaona vyema Bwana, huninyeshei?
Na mimi? Na mimi? Bwana, huninyeshei?
2. Sinipite, Baba Mwema; dhambini nimezama;
Rehema niza daima; Bwana hunionyeshi?

3. Sinipite, Yesu Mwema; niwe nawe daima,
Natamani kukwandama: Bwana, hunichukui?

4. Sinipite, Roho Mwema, Mpaji wa uzima,
Nawe shahidi wa wema, Bwana wema hunipi?

Nyimbo Za Kikristo No. 40: Nijaze Sasa

1. Njoo, Roho Mtukufu uoshe moyo wangu,
Utakase nia yangu, njoo, nijaze sasa.
Roho Mtukufu, njoo, nijaze sasa;
Utakase nia yangu, njoo, nijaze sasa.
2. Unijaze moyo wangu Ijapo sikuoni,
Nami ninakuhitaji, njoo, nijaze sasa.

3. Nimejaa udhaifu, nainamia kwako;
Roho Mtukufu sasa, nitilie na nguvu.

4. Unioshe nifariji niponye, nibariki,
Unijaze moyo wangu; ndiwe mwenye uwezo.
 

Nyimbo Za Kikristo No. 21 - 30

Nyimbo Za Kikristo No. 21: Baba Twakujia
  1. Bwana twakujia, Uwe msaada;                                                                                                    Uwe kimbilio, twakusihi.
    Dunia ni giza tukitengwa nawe;
    Tufariji hapa, baba yetu.
Baba teakujia, tu dhaifu, usitugeue, tusikie.
  1. Salama tulinde, kati ya taabu;                                                                                                       Uwe raha yetu mashakani.
    Roho yasumbuka, Baba tujalie;
    Twakuomba sana, tupe nguvu.
  1. Neema utupe, tukubali kwako;                                                                                                  Moyo wetulinda, safarini;
    Tuongoe mbele, tupate kushinda
    Na kufika ng'ambo, kule kwako.
Nyimbo Za Kikristo No. 22:
  1. Usinipite, Mwokozi, unisikie;                                                                                              Unapozuru wengine, usinipite.
    Bwana, Bwana unisikie;
    Unapozuru wengini, usinipite.
  1. Kiti chako cha rehema, nakitazama;                                                                                               Magoti napiga pale, nisamehewe.
  1. Sina ya kutegemea, ila wewe tu;                                                                                                   Uso wako uwe kwangu: nakuabudu.
  1. Wewe tu u Mfariji: sina mbinguni,                                                                                                Wala duniani pote, Bwana mwingine.
Nyimbo Za Kikristo No. 23: Yesu Furaha Ya Moyo
  1. Yesu, furaha ya moyo! Hazina ya pendo, na nuru.                                                                                Yote yatupendezayo, yasilinganishe nawe.
  1. Kweli yako ya daima, wawajibu wakwitao,                                                                                     Ni siku zote u mwema kwao wakutafutao,.
  1. U mkate wa Uzima, kupokea ni baraka,                                                                                  Twanya kwako u kisima roho zikiburudika.
  1. Mwokozi twakutamani, kwako roho hutulia;                                                                     Twakushika kwa imani, nawe watubarikia.
  1. Yesu, ndiwe kwetu mwanga, tufurahishe daima;                                                                            Giza ya dhambi fukuza, uwe mwanga wa Uzima.
Nyimbo Za Kikristo No. 24: Jina La Yesu Tamu
  1. Jina lake Yesu tamu Tukilisikia,                                                                                            Hutupoza, tena hamu Hutuondolea.
  1. Roho ilioumia Kwalo hutibika,                                                                                                Chakula, njaani pia; Raha, tukichoka.
  1. Jina hili ni msingi, Ngao, ngome, mwamba,                                                                                   Kwa hili napata ungi, Kwangu ni akiba.
  1. Yesu, Mchunga, Rafiki, Mwalimu,                                                                                  Kuhani,Mwanzo, mwisho, na amina, mali yangu yote!
  1. Moyo wangu hauwezi Kukusifu kweli;                                                                                             Ila sifa zangu hizi, Bwana, zikubali.
Nyimbo Za Kikristo No. 25: Taji Mvikeni
  1. Taji mvikeni. Taji nyingi sana,                                                                                                 Kondoo mwake Kitini, Bwana wa mabwana;
    Nami tamsifu Alikufa kwangu,
    Ni Mfalme mtukufu, Seyidi wa mbingu.
  1. Taji mvikeni Mwana wa Bikira;                                                                                            Anazovaa kichani Aliteka nyara;
    Shilo wa manabii Mchunga wa watu
    Shina na tanzu ya Yesu wa Bethliehemu.
  1. Taji mvikeni Bwana wa Mapenzi;                                                                                              Jeraha zake ni shani Ni vito nya enzi,
    Mbingu haina Hata malaika
    Awezae kuziona pasipo kushangaa!
  1. Taji mvikeni Bwana wa Salama;                                                                                                  Kote - kote duniani Vita vitakoma;
    Nayo enzi yake itaendelea,
    Chini ya miguu yake, Maua humea.
Nyimbo Za Kikristo No. 26: Tutokapo Tubariki
  1. Tutokapo tubariki, Utupe kufurahi;                                                                                              Tuwe na upendo wako, Neema ya kushinda.
    Nawe utuburudishe tukisafiri chini.
  1. Twatoa sifa, shukrani Kwa neno la injili;                                                                                  Matunda yake wokovu Yaonekane kwetu;
    Daima tuwe amini Kwa kweli yako, Bwana.
  1. Siku zetu zikizidi Tuzitoe kwa Yesu;                                                                                            Tuwe na nguvu moyoni Tusichoke njiani;
    Hata tutakapoona Utukufu wa Bwana.
Nyimbo Za Kikristo No. 26a: Tupe Amani
  1. Mungu mtukufu Aliyeumba pepo kuvuma Na radi kali;                                                                  Toa neema unapotawala, Tupe amani Bwana wa wema.
  1. Mungu wa neema, Nchi imeacha Amri tukufu Na Neno lako;                                                     Hasira zako Zisituharibu, Tupe amani, Bwana wa wema.
  1. Mwumbaji wa haki, Watu wabaya Wamedharau Utukufu wako;                                                Lakini wema wako Utadumu; Endesha kweli Bwana wa wema.
  1. Tunakutolea Ibada safi Kwa ajili ya Wokovu wako;                                                                      Hivi tunaziimba Sifa zako; Wako uwezo Na utukufu.
Nyimbo Za Kikristo No. 27: Tena, Mwokozi, Twalitukuza Jina Lako
  1. Tena, Mwokozi, twalitukuza                                                                                                          Jina lako lenye kupendeza,
    Twangojea neno la amani,
    Kabla hatujakwenda nyumbani.
  1. Tupe amani njiani mwetu,                                                                                                          Wewe u mwanzo, u mwisho wetu;
    Dhambini kamwe isiingie
    Midomo ikitajayo wewe.
  1. Utupe amani usiku huu,                                                                                                                    Ili gizani kuwe nuru kuu.
    Tulinde kwa kuwa kwako Bwana.
    Usiku ni sawa na mchana.
  1. Tupe amani ulimwenguni                                                                                                             Ndiyo dawa yetu majonzini;
    Na ikitwita sauti yako,
    Tupe amani milele kwako.
Nyimbo Za Kikristo No. 28: Jina La Thamani
  1. Jina lake Yesu tamu, Lihifadhi moyoni;                                                                                         Litatufariji ndugu, Enda nalo po pote.                                                                                                                                                                                                                                                           Jina la (Thamani) thamani, (thamani) Tumai la dunia                                                                        Jina la (Jina la thamani-tamu!) thamani,Furaha ya mbinguni.
  1. Jina la Yesu lafaa Kama ngao vitani,                                                                                                Majaribu yakisonga, Omba kwa jina hili.
  1. Jina hili la thamani Linatufurahisha,                                                                                            Anapotukaribisha, Na tunapomwimbia.
  1. Mwisho wa safari yetu Tutakapomsujudu,                                                                                     Jina hili tutasifu Furaha ya mbinguni.
Nyimbo Za Kikristo No. 29: Yesu, Nakupenda
  1. Yesu nakupenda, U mali yangu,                                                                                                           Anasa za dhambi sitaki kwangu;
    Na mwokozi aliyeniokoa 
    Sasa nakupenda, kuzidi pia.
  1. Moyo umejaa mapenzi tele                                                                                                          Kwa vile ulivyonipenda mbele,
    Uhai wako ukanitolea
    Sasa nakupenda, kuzidi pia.
  1. Ulipoangikwa Msalabani                                                                                                         Tusamehewe tulio ndambini;
    Taji ya miiba uliyoivaa,
    Sasa nakupenda, kuzidi pia.
  1. Mawanda mazuri na masikani                                                                                               Niyatazamapo huko mbinguni,
    'Tusema na taji nitakayovaa
    Sasa nakupenda, kuzidi pia.
Nyimbo Za Kikristo No. 30: Yesu, Unipendaye
  1. Yesu unipendaye kwako nakimbilia,                                                                                                Ni wewe utoshaye mwovu akinijia.
    Yafiche ubavuni mwako maisha yangu;
    Nifishe bandarini, wokoe moyo wangu.
  1. Ngome nyingine sina; nategemea kwako,                                                                              Usinitupe Bwana, nipe neema yako,
    Ninakuamania, mwenye kuniwezesha;
    Shari wanikingia, vitani wanitosha.
  1. Nakutaka Mpaji, vyote napata kwako;                                                                                   Niwapo muhitaji, utanijazi vyako;
    Nao waangukao wanyonge wape nguvu;
    Poza wauguao, uongoze vipofu.
  1. Mwana umeniosha moyo kwa damu yako;                                                                               Neema ya kutosha yapatikana kwako;
    Kwako Bwana naona kisima cha uzima;
    Mwangu moyoni, Bwana, bubujika daima.