Monday, November 3, 2014

Nyimbo Za Kikristo: 71-80

71. Kesheni Kaombeni
Watch, For The Time Is Short

1. Kesha ukaombe panapo mafasi; Wakati si mwingi. Kwa vile ukeshe
Mwili ni dhaifu. Adui hodari karibu atakuja, Bwana wa arusi.

Kesha, Omba, Kesha, Omba,
Kesha Kaombe gizani, mchana,
Daima kesha.

2. Fukuza usingizi, fukuza mashaka; Ahadi ni yako, raha ya milele
Bwana alkesha kwa ajili yako; Jasho yeke ikawa matone ya dame.

3. Yesu umkubali awe nguvu zako; silaha uzivae; adui karibu.
Sasa nafasi iko, isipite bure; Bila kukawia masihiya kesha.

72.Jenga Juu Ya Mwamba
We'll Build on the Rock

1. Tutajenga juu ya mwanba wa Yesu, Mwamba wa kale;
Tutavumilia kishindo tufani ivumapo.

Tutajenga juu, (Tutajenga juu ya mwamba mkuu)
Tutajinga juu, (Tutajenga juu ya mwanba mkuu)
Tuta jenga juu ya mwamba mkuu, juu yake Yesu.

2. Wingine hujenga katika Mchanga wa ulimwengu;
Wingine katika mawimbi ya anasa za dhambi.

3. Jenga nawe juu ya mwanba, Msing pekee wa kweli:
Tumaini lake litadume, tumai la wokovu.

73. "Bwana, Uniongoze Juu"
I'm Pressing On

1. Nakaza mwendo mbinguni, kila siku napanda juu;
Naomba nikisafiri, "Bwana uniongoze juu.

Bwana uniinue juu Kwa imani hata mbingu,
Juu kuliko dunia; Bwana uniongoze juu.

2. Moyo wangu hutaki Kukaa palipo shaka;
Wengine wapenda chini nia yangu ni ku panda.

3. Nataka kupanda juu Nisishindwe na adui;
Kwa imani nasikia sauti ya washindaji.

4. Kupanda juu nataka niuone utukufu;
Hata mwisho nitaomba, "Bwana uniongoze juu."

74. Niambie, Ee Mlinzi
Watchman, Tell Me

1. Niambie, Ee mlinzi, Umepambazuka je!
Utukufu wa Zayuni; Pana dalili zake?
Msafiri uondoke, Utazame mbinguni,
Kiunoni ujifunge, Ni kucha, alifajiri.

2. Mlinzi, inamurika nuru njiani mwako,
Dalili ya kuja kwake, Kwamba siku karibu;
Panda itakapolia Itawaamsha wafu,
Watakatifu wa Mungu, Kuwapa kutokufa.

3. Mlinzi, ione nuru Ya mwaka wa Sabato;
Sauti zina tangaza Ufalme ni karibu:
Msafiri ninaona mlima wa Zayuini,
Mji wa Yerusalemu nayo fahari yake.

4. Kwenye mji wa dhahabu Anaketi Mfalme
Katika kiti kizuri: Huku ana tawala.
Pana amani po pote, Mashamba husitawi;
Na srdhi ina rutuba; Mito ni mitulivu.

5. Mlinzi, twakaribia Nchi iliyo nzuri;
Twende mbele, tufurahi, Nchi inachangamka.
Sikieni kuna wimbo Wa waliookoka;
Kaza mwendo, Ujiunge na kundi kubwa hili.

75. Msingi Imara, Ninyi Wa Bwana
How Firm a Foundation

1. Msingi imara, ninyi wa Bwana,
Ume wekwa kwenu kwa neno lake?
Nini zaidi atasema Bwana?
Imani yenu ipate kuzidi?

2. Wanbiwapo vuka maji ya giza,
Mito ya mashaka haitazidi;
'Takuwapo nawe, nikuwezeshe,
Shida upatazo zisikutishe!

3. Utakapopishwa Ndani ya moto
Nguvu nitakupa, upate pato;
Huteketezwi, ila taka zako.
Na zitasalia dhahabu zako.

4. Na mtu aliyenitegemea
Nguvu za jehanamu zijapotisha,
Kamwe kwa adui sitamtia;
Mtu wangu kamwe sitamuacha.

76. Mrithi Ufalme
Heir of the Kingdom

1. Mrithi ufalme kwani walala?
Karibu wokovu wasinzia?
Amka simama uvae silaha
Haraka sana saa zapita.

2. Mrithi ufalme mbona 'kawia'?
M-bona hupokei zawadi?
Haya uvae, Mwokozi yuaja;
Haraka, umlaki apitapo.

3. Mataifa makuu ya dunia
Yapigana na kujiangusha.
Usiziofu dalili, Mrithi;
Ishara zotte hazikawii.

4. 'Sitazame anasa za dunia!
Kwani hayo ya pita upesi.
Zivunje kamba zinazokufunga.
Mrithi ufalme, njoo'karudi.

5. Inua kichwa, tazama mbele tu.
M-falme aja na utukufu;
Jua la onekana milimani,
Warithi ufalme furahini.

77. Habari Za Usiku
Watchman on the Walls of Zion

1. Je! Mkinzi ukutani
Wa mji wa Zayuni,
Habari zake usiku?
Asubuhi karibu?
Kuna dalili za kupambazuka?
Kuna dalili za kupambazuka?

2. Katika safari yetu
Twaona nchi kavu?
Tutalala baharini?
Bandari bado mbali?
Kweli, kweli tutaona ufalme?
Kweli, kweli tutaona ufalme?

3. Tunaona nuru yake
Nyota ya asubuhi;
Nyota, tukufu na safi
Inang'aa mbinguni;
Furahini, wokovu u karibu.
Furahini, wokovu u karibu.

4. Tumetazama ramani,
Kweli pwani si mbali;
Twende mbele, kwa upesi
Tutaona bandari;
Furahini, imbeni nyimbo zenu.
Furahini, imbeni nyimbo zenu.

78.Mpaka Lini Bwana
How Long, O Lord our Saviour

1. Mpaka lini Bwana 2.Mpaka lini, Yesu,
Utakaa mbali? Utaacha watu
Kemetuchosha moyo Uliowakomboa
Kukawia hivi. Wawe na mashaka?
Utatujia lini, Wachache waamini
Ili tu furahi Kwamba utarudi;
Katika ile nuru, Wachache wa tayari
Kuja kutukufu? Bwana Kukulaki

3.Waamshe watu wako;
Tangaza kilio:
"Mwe watakatifu,
Bwana yu Karibu!"
Utatujia lini,
Ili tu furahi
Katika ile nuru,
Kuja kutukufu?

79. Nataka Imani Hii
O For a Faith

1. Nataka Imani hii: Imani imara
Ambayo haitetemi Kitu chote Wakati wa shida,
Wakati wa shida.

2. Isiyonung'unika Huzuni, taabu;
Lakini katika saa ya matata Humwamini Mungu,
Humwamini Mungu.

3. Imani inayo ng'aa katika tufani;
Isiyoogopa giza, wala shida, Njaa na Hatari,
Njaa na hatari.

4. Haiogopi dunia, Kudharau kwake;
Haiangushwi na hila, na uwongo Dhambi na ogofyo,
Dhambi na ogofyo.

5. Bwana, nipe imani hii, Hivi nita weza
Kuonja hapa chini ulimwenguni, Kurithi furaha,
Kurithi furaha.

80. Tupe Moto Wa Uhai
O For That Flame of Living Fire

1. Tupe moto wa uhai Uliowaka zamani,
Uliowaongoza juu Wazee watakatifu.

2. Wapi roho iliyokaa Moyoni mwa Ibrahimu?
Kadhalika ndugu Paulo Aliwezeshwa na moto.

3. Neema yako haina Nguvu siku hizi sawa
Kama wakati wa Musa, Ayubu na wa Eliya?

4. Zamani za kale, Bwana, Kumbuka na kwa rehema,
Zihuishe roho zetu Kwa Roho Mtakatifu.

No comments:

Post a Comment