Monday, November 3, 2014

Nyimbo Za Kikristo: 141-160

141. Chini Ya Msalaba
Beneath the Cross of Jesus

1. Chini ya msalaba Nataka simama;
Ndio mwamba safarini, Wa kivuli chema;
Ni kweli kwa roho yangu Ni tuo kamili,
Tatua mziho wangu Wakati wa hari.

2. Hapa ni pema sana, Ni ngome kamili;
Hapa yameonekana, Mapenzi ya kweli;
Kama alivyoonyeshwa Yakobo zamani,
Msalaba umekuwa ngazi ya mbinguni.

3. Na Yesu Msalabani Walimkimea,
Alikufa niokoke Niliyepotea:
Naona ajabu sana Ya manbo mawili
Jinsi alivyonipenda Nisiyestahili.

4. Atakayeonana Na Yesu mbinguni,
Njia yake aanzapo Ni Msalabani;
Wokovu upo hapa tu, Mwingine hapana,
Kisha kuna furaha kuu Pamoja na Bwana.
142. Nasikia Sauti Yako
I hear Thy Welcome Voice

1. Nasikia mwito, Ni sauti yako;
Nikasafiwe kwa damu Ya kwangikwa kwako.

Nimesongea mtini pako,
Unisafi kwa damu ya kwangikwa kwako.

2. Ni mnyonge kweli, umenipa nguvu;
Ulivyonisfi taka Ni utimilivu.

3. Yesu hunijuvya: Mapenzi imani,
Tumai, amani, rahi, hapa na mbinguni.

4. Napata wokovu, Wema na neema;
Kwako Bwana nina nguvu Na haki daima.





143. Naamini
Father, I Stretch My Hands

1. Baba sina msaada ila kwako pekee;
Kama kwangu ungefichwa, Nifanyeji, Baba?

Sasa hivi naamini Yesu alikufa,
Aliimwaga damu yake, Nitoke dhambini.

2. Naamini mwana wako Nipe nguvu zako;
Nijazie mahitaji, katika saa hii.

3. Nifuraha gain kwangu kukuona uso!
Nijue sauti yako, Nipate neema.

144. Ni Wako Bwana
I am Thine O Lord

1. Ni wako Bwana, ninasikia Unaponena nami;
Lakini, kweli, nataka kwako Nizidi kusongea.

Bwana vuta, (vuta) nije nisongee
Sana kwako mtini.
Bwana, vuta, vuta, nije nisongee
Pa damu ya thamani.

2. Niweke sasa nikatumike kwa nguvu za neema;
Uyapendayo nami nipende Nizidi kukwandama.

3. Nina furaha tele kila saa nizungumzapo nawe;
Ninanena kama kwa rafiki Nikipiga magoti.

145. Namtaka Bwana Yesu
Take The World

1. Ulimwengu siutaki, Namtaka Bwana yesu;
Dunia hunidanganya; yesu yu mwaminifu.

Rehema ni ya ajabu! Pendo bila kipimo!
Wokovu mkamilifu, Amana ya uzima.

2. Ulimwengu siutaki, Namtaka Bwana yesu;
Kati ya dhoruba kali Yeye wimbo mtamu.

3. Ulimwengu siutaki, namtaka Bwana yesu;
Safarini duniani Yeye furaha yangu.

4. Ulimwengu siutaki, Namtaka Bwana yesu;
Msalaba naamini, Hata Namwona Yesu.

146. Twae Wangu Uzima
Take My Life and Let It Be

1. Twae wangu uzima sadaka ya daima;
Twae saa na usiku Zikutukuze huku.

2. Twae mikono nayo, ifanye upendayo,
Twae yangu miguu, Kwa wongozi wako tu.

3. Twae sauti yangu, niimbe kwa Mungu tu;
Itwae na midomo, Ijae neno lako.

4. Twae dhahabu pia Na yote ya dunia;
Twae yangu hekima, upendavyo tumia.

5. Nia itwae, Mungu, haitakuwa yangu;
Twae moyo; ni wako, uwe makazi yako.

6. Twae mapenzi yangu, sifa za moyo wangu;
Twae kabisa nafsi Niwe wako halisi.

147. Uishi Ndani Yangu
Love Out Thy Life Within Me

1. Tawala ndani yangu, Ee Yesu, Mfalme.
Uwe kwangu majibu kwa maswali yangu;
Uishi ndani yangu, Wewe, mwongozi
Utumishi ni wangu, Wako utukufu.

2. Hekalu nimetoa, Umelisafisha;
Sasa fahari yako Imulike ndani;
Dunia iwe kumya, mwili sasa uwe
Mtumwa mtulivu Wa kukutii tu.

3. Viungo vyake mwili, Vyote vikungoja
Tayari vikuutwa Kwenda, kusimama;
Bila manumguniko au malaumu,
Au kusumbuliwa, Pasipo majuto.

4. Niwe na utulivu pasipo haraka;
Tayari kungojea maagizo yako.
Tawala ndani yangu, Ee Yesu, Mfalme,
Uwe kwanfgu majibu kwa maswali yote.

148.Univute Karibu
Closer to Thee, My Father, Draw Me

1. Univute karibu, Baba, Unikumbatie;
Unisogeze kifuani, Nataka pumziko.

Univute karibu(Vuta, univute karibu)
Kwa kamba za upendo, (Kwa kamba, kamba za upendo)

Univute (kwa kamba za upendo, Univute karibu)
Karibu nawe. (Univute karibu)

2. Univute Mwokozi wangu, Na tusiachane;
Mikono yako juu yangu Leo nione.

3. Univute kwa Roho yako, Nifanane nawe;
Unioshe, unihuishe, Niwe safi, huru.

149. Kuwa Wake Yesu
Would You Live for Jesus

1. Kuwa wake Yesu, je! Ni kusudi lako?
Ungeenda naye njia nyembamba?
Unataka aubebe mzigo wako?
Awe Mwongozi wako.

Uwezo wake unakutosha
Na danu yake itakusafi;
Kwa vile ukubali ni bora
Afanye mapenzi yake nawe

2. Unataka kutika unapokwita?
Kupata amani kwa kumpa vyote?
Wataka uwezo usianguke kamwe?
Awe Mwongozi wako.

3. Wataka raha katiak ufalme wake?
Ungeshinda kwa majaribu yote?
Ungefanya kazi yake vizuri sana?
Awe Mwongozi wako.

150. Hasha Maneno Mabaya Yasitoke
Angry Words! Oh, Let them Never

1. Hasha, maneno mabaya yasitoke kinywani
Moyo mwema uzuie Ndimi, zisichafuke.

"Nanyi pendeni", Asema yesu,
(Mpendane) (Mpendane)
Kama mwanzo alivyotupenda:
"Nanyi pendeni", alivyotupenda:
(Mpendane) (Mpendane)
Wana, tiini amri hii. (amri heri hii).

2. Pendo ni mtakatifu; Urafiki; mzuri:
Visiharibike mara kwa kunena vibaya.

3. Tusinene kwa hasira, inazaa huzuni,
Pendo lako ee mwokozi, Inatosha tushindi.

151. Huniongoza Mwokozi
He Leadeth Me

1. Huniongoza Mwokozi, ndipo nami hufurahi,
Niendapo pote napo, ataniongoza papo.

Kuongoza hunishika; kwa mkono wa hakika;
Nitaandamana naye Kristo aniongozae.

2. Pengine ni mashakani nami pengine rahani;
Ni radhi, ijayo yote, yupo nami siku zote.

3. Mkono akinishika kamwe sitanung'unika;
Atakachoniletea ni tayari kupokea.

4. Nikiisha kazi chini sita kimbia mauti;
Kushinda ni ya hakika nikiongozwa na Baba.

152. Karibu Na Wewe, Mungu Wangu
Nearer, My God, to Thee

1. Karibu na wewe, Mungu wangu:
Karibu zaidi Bwana wangu,
Siku zote niwe karibu na Wewe,
Karibu zaidi, Mungu wangu.

2. Mimi nasafiri duniani,
Pa kupumzika sipaoni,
Nilalapo niwe karibu na Wewe,
Karibu zaidi, Mungu wangu.

3. Yote unipayo yanivuta;
Pa kukaribia nitapata;
Na nielekezwe, karibu na Wewe,
Karibu zaidi, Mungu wangu.

4. Na kwa nguvu zangu nikusifu;
Mwamba, uwe maji ya wokovu
Mashakani niwe kaaribu na Wewe;
Karibu zaidi, Mungu wangu.

5. Na nyumbani mwa juu, Baba yangu
Nikinyakuliwa toka huko,
Kwa furaha niwe pamoja na Wewe,
Karibu zaidi, Mungu wangu.




153. Fikira Moja Tu
One Sweetly Solemn Thought

1. Fikira moja tu
Hurejea tena
Nimekaribia mbingu
Zaidi ya jana.

Karibu na kwetu mbingu,
Karibu na kwetu sasa,
Nikwone karibu.

2. Karibu na kwetu
Na kwenye makao;
Kiti cha enzi cha Mungu,
Pahali pa mto.

3. Kamilisha Yesu,
Kuamini kwangu;
Nikifika mwisho wangu,
Nikwone karibu.

154. Yanipasa Kuwa Naye
I Must Have The Saviour With Me

1. Yanipasa kuwa naye, Mwokozi Bwana wangu,
Akiwa karibu nami, napata nguvu kweli.

Moyo hauogopi, wala kitikisika.
Nitakwenda apendapo. Kwa kuwa anilinda.

2. Yanipasa kuwa naye, kwani nategemea;
Anaweza kufariji na maneno matamu.

3. Yanipasa kuwa naye maisha yangu yote;
Yakiwapo majaribu na mashaka yo yote.

4. Yanipasa kuwa naye katika njia zangu;
Macho yake yaongoza hatua zangu zote.

155. Njiani Huniongoza
All the Way my Saviour Leads Me

1. Njiani huniongoza. Yesu wangu, Mwokozi;
Rehema hatapunguza, Milele Kiongozi.
Ina raha kwandamana Duniani daima;
Nijaposumbuka sana, Yeye hutenda vyema,

2. Njiani huniongoza Hupunguza matata;
Nikiugua hupoza, Na njaani nashiba.
Lichokapo guu langu Nguvu zikapungua,
Jiwe lilo mbele yangu Hunibubujikia.

3. Njiani huniongoza Kwa pendo zilizo kuu,
Mwisho atanituliza Kwake Baba yangu juu.
Nikivikwa kutokufa, Nikae na Mwokozi,
Nitamsifu sana; sifa: "Kweli ni Kiongozi."

156. Uniongoze, Yehova
Guide Me, O Thou Great Jehovah

1. Uniongoze, Yehova, Ni msafiri chini;
Ni mnyonge, u hodari, 'Nilinde kwa mkono.
Unitunze, unilinde, Unionyeshe njia!

2. Na kisima cha uzima, Maji ya utabibu,
Fungua kwa moyo wangu, Ninywe na kuponyeka!
Uninyweshe, unilishe, Hata nimetosheka.

3. Wakati wa kuuvuka, Ule mto Yordani,
Hofu yangu ufariji, 'Nione uso wako.
Nyimbo shangwe, nyimbo shangwe, Nitaimba daima.

157. Mfalme Yu Mlangoni
The Coming King

1. Mfalme yu mlangoni, Ndiye aliyetufia;
Mara wote wampendao atawakusanya.

Yuaja, yuaja, mlangoni anasimama;
Anakuja, anakuja, Kuja kwake karibu.

2. Dalili za kuja kwake Zinazidi kutimizwa;
Karibu wateule watamlaki Bwana.

3. 'Sitafute duniani amani wala furaha,
Mpaka Bwana arudi dhambi kuondoa.

4. Tutakaa na Mwokozi Makaoni ya milele;
Daima tutafurahi kuwa watu wake.

158. U Mwendo Gani Nyumbani?
How Far From Home?

1. U mwendo gani nyumbani? Mlinzi akanijibu,
"Usiku sasa waisha,mahe kaibu."
Usihuzunike tena, bali ulemee mwendo
Hata ushike ufalme kule mwangani juu.

2. Na tena niliuliza, nchi yote ikajibu:
"Sasa mwendo watimika, milele karibu."
Usihuzunike tena, ishara kuu zasonga
Na viumbe vyangojea sauti ya Bwana.

3. Nikamwuliza shujaa, ndivyo kanitia moyo:
"Shikilia mapigano, kitambo yaisha."
Usihuzunike tena, kazi ifanye kwa moyo;
Tumeahidiwa tunu tuishapo shinda.

4. Siyo mbali na nyumbani! Fikara tamu njiani,
Latupoza roho, nalo lafuta machozi
Usihuzunike tena, kitambo tutakutana
Wenye furaha kamili nyumbani mwa Baba.









159. Anakuja Upesi
How Sweet are the Tidings

1. Anakuja upesi, Yesu Bwana wetu, Msafiri mbali na kwao;
Alisema dhahiri, "Nitakuja tena"; Amina; na uje, E Bwana.

Yuaja, Yesu atarudi sasa; Anakuja duniani.
Wasafiri wote watapumzika Yesu anaporudi tena.

2. Makaburi yote wafu wanapolala Yatafunguliwa tena;
Na mamilioni pale wataondoka tena, Wasione machozi kamwe.

3. Hatutatengana na hao tena huko; Nyimbo nzuri tutaimba.
Watakusanyika 'toka kila kabila, Miguuni pa Mwana-kondoo.

4. Aleluya Amin! Aleluya tena! Upendo wake unashinda!
Tutamsifu milele, hata tutashangaa, Jinsi alivyo tukomboa.

160. Watakatifu Kesheni
Watch, Ye Saints

1. Watakatifu kesheni, nguvu za mbingu zagonga;
Washeni taa tayari kwa kurudi kwake Bwana.

Yuaja, Yesu Mfalme, Yuaja myenye fahari,
Yesu yuaja enzini. Karibu Yesu, uje.

2. Piga mbiu, tangazeni habari ya ukombozi,
Ya mponya wa upendo nayo nguzu za samaha.

3. Falme nyingi zaangushwa, Panda ya saba hulia;
Tangaza neema yake kabla ya kupita saa.

4. Mataifa yapotea, nchi zajaa uchungu:
Kistro anaharakisha, Unabii unatimizwa.

5. Wenye dhambi njoni sasa, Kristo awapatanishe,
Mbio twaeni neema, kitambo muda waisha.

No comments:

Post a Comment