Saturday, November 24, 2012

Nyimbo Za Kikristo 51 - 60

Nyimbo Za Kikristo No. 51: Kuwa Na Yesu

 

1.      Yesu Mwokozi, kwa hakika, Hunipa furaha na amani;
Mrithi wa wokovu wake, Natakaswa kwa damu yake.

 

Habari hiyo wimbo wangu, Daima nitamsifu Yesu.
Habari hiyo wimbo wangu, Daima nitamsifu Yesu.

 

2.      Nijitoapo nina raha, Na kwa imani namwona Bwana;

Aniletea malaika, Wananilinda, niokoke.

 

3.      Hali na mali anaitwaa, Katika Yesu nabarikiwa;
Nikimngoja kwa subira, Wema wake unanitosha.

 

Nyimbo Za Kikristo No. 52: Nipe Biblia

 

1.      Nipe Biblia nyota ya furaha, wapate nuru wasafirio;
Hakuna la kuzuia amani,
Kwani Yesu alituokua.

 

Nipe Biblia neno takatifu,
Nuru yake itaniongoza;
Sheria na ahadi na upendo,

Hata mwisho vitaendelea.

 

2.      Nipe Biblia nihuzunikapo ikinijaza moyoni dhambi;
Nipe neno zuri la Bwana Yesu,
Nimwone Yesu Mwokozi wangu.

 

3.      Nipe Biblia nipate kuona, hatari zilizo duniani;
Nuru ya neno lake Bwana Yesu,
itaangaza njia ya kweli.

 

4.      Nipe Biblia taa ya maisha; Mfariji tunapofiliwa;
Unionyeshe taa ya mbinguni,
Nione utukufu wa Bwana.

 

Nyimbo Za Kikristo No. 53: Napenda Kuhubiri!

 

1.      Napenda kuhubiri habari ya Yesu,
Ya Bwana wa fahari na pendo zake kuu.
Huhubiri napenda kwa hali na mali;
Mwenyewe Nimeonja najua ni kweli.


Napenda kuhubiri kisa cha Bwana Yesu,
Ya Bwana wa fahari na pendo Zake Kuu.

 

2.      Napenda kuhubiri mambo ya ajabu
Na tukiyatafikiri yapita Dhahabu.
Kuhubiri napenda ya yaliyonifaa;
Nami sana napenda hayo kukwambia.

 

3.      Napenda kuhubiri, hunifurahisha
Tamu yake habari haiwezi kwisha.
Napenda kuhubiri wa gizani nao;
hawana muhubiri wa kweleza chuo.

 

4.      Kuhubiri napenda hata wajuao;
Kusikia hupenda kama wenzi wao.
Nako kwenye fahari nikiimba wimbo
Nitaimba habari ya Mwokozi huyo!

 

Nyimbo Za Kikristo No. 54: Nataka Nimjue Yesu!

 

1.      Nataka nimjue Yesu, na nizidi kumfahamu,
Nijue pendo lake tu, wokovu wake kamili.

 

Zaidi zaidi, nimfahamu Yesu,
Nijue upendo wake, wokovu wake kamili.

 

2.      Nataka nimjue Yesu, na nizidi kusikia

Anenapo kitabuni, kunidhihirisha kwangu.

 

3.      Nataka tena zaidi, daima kupambanua
Mapenzi yake, nifanye yale yanayompendeza.

 

4.      Nataka nikae, kwa mazungumzo matamu.
Nizidi kuwaonyesha wengine wokovu wake!

 

Nyimbo Za Kikristo No. 55: Twapanda Mapema

 

1.      Twapanda mapema, na mchana kutwa

Mbegu za fadhili hata jioni,

Twangojea sasa siku za kuvuna;

Tutashangilia wenye mavuno.

 

Wenye mavuno, wenye mavuno,

Tutashangilia wenye mavuno.

Wenye mavuno, wenye mavuno,

Tutashangilia wenye mavuno.

 

2.      Twapanda mwangani na kwenye kivuli;

Tushindwe na baridi na pepo;

Punde itakwisha kazi yetu hapa:

Tutashangilia wenye mavuno.

 

3.      Twapanda kwa Bwana mbegu kila siku.

Tujapoona taabu na huzuni;

Tuishapo shinda atatupokea:

Tutashangilia wenye mavuno.

 

Nyimbo Za Kikristo No. 56: Waponyeni Watu

 

1.      Walio kifoni, nenda waponye.

Uwatoe walio shimoni;

Wanaoanguka uwainue;

Habari njema uwajulishe.

 

Walio kifoni waokoeni,

Mwokozi yuko huwangojea.

 

2.      Wajapokawia anangojea,

Awasubiri waje tobani;

Mwokozi hawezi kuwadharau,

Huwasamehe tangu zamani.

 

3.      Na ndani ya moyo wa wanadamu

Hawamo shida, tena huzuni;

Lakini kwa Yesu huna rehema

Kuwaponya na kuwaokoa.

 

4.      Walio kifoni, nenda waponye

Kazi ni yetu, zawadi iko;

Nguvu kuhubiri Bwana hutoa

Kwa subira tuwavute sasa.

 

Nyimbo Za Kikristo No. 57: Usikatae Kazi

 

1.      Usikatae Kazi yake Bwana; Ukae tayari Kuifanya kazi;

Uende po pote Mungu akwitapo, Nawe utaona Furaha kazini.

 

Njoo, We! Usiikatae; Njoo, We! Uifanye kazi;

Usiikatae Kazi yake Bwana, Ili hatimaye usikatazwe juu.

 

2.      Usiikatae Kazi yake Bwana; Kwa nini kawia? Fanya kazi leo.

Mavuno meupe, Wachache Wavuni, Onyesha furaha Kwa kazi ya Bwana.

 

3.      Usiikatae Kazi yake Bwana, Kukataa pendo Kwako ni Hatari.

Saa ya rehema, Yesu akiomba, Ziungame dhambi, Zifutwe mbinguni.

 

Nyimbo Za Kikristo No. 58: Zitakuwa Nyota Tajini?

 

1.      Leo ninafikiri ya nchi nzuri Ninayotaka kuiona;

Nisimamapo karibu na Mwokozi, Tajini zitakuwa nyota?

 

Sijui tajini mwangu kama nyota

Zitang'aa kila wakati!

Nitakapoamka katika majumba,

Zitakuwa nyota tajini?

 

2.      Kwa nguvu za Bwana nitafanya kazi, Nitavuta roho za watu,

Ili niwe na nyota katika taji, Bwana anapotupa tunu.

 

3.      Nitakuwa na furaha nikimwona, Kuweka miguuni pake

Watu waliovutwa kwa ajili ya Kazi yangu na Roho yake.

 

Nyimbo Za Kikristo No. 59: Fanyeni Kazi Zenu

 

1.      Fanyeni kazi zenu, usiku si mbali;

Kesheni saa zenu vumilieni:

Kwa Yesu tumikeni na hiyo Injili.

Sana wahubirini watu wa mbali.

 

2.      Fanyeni kazi zenu giza yasongea;

Na wengi wenzi wenu wamo gizani.

Msipoteze moja dakika ni hizi;

Mwana atarejea mwisho wa kazi.

 

3.      Fanyeni kazi zenu, hivi jua lachwa;

Wote walio kwenu apenda Mungu:

Na sisi tumjuaye na tuwafundishe,

Ili Yesu ajaye tumfurahishe.

 

Nyimbo Za Kikristo No. 60: Nitakwenda Utakaponituma

 

1.      Pengine sio milimani Utakaponiita;

Pengine siyo baharini wala palipo vita;

Lakini, nitajibu, na njia siijui.

Bwana, nitajibu, ni tayari Kwenda uniagizapo.

 

Ukiwa pamoja nami, Bwana, Mlimani, baharini,

Niende utakaponiita; Na fuata uendeko.

 

2.      Pengine leo kuna neno, Neno tamu la pendo,

Ambalo Yesu anataka Ninene kwa upole;

Ukiwa pamoja nami, Bwana, Nitamtafuta leo

Yule aliyepotea mbali: Nitasema upendavyo.

 

3.      Pahali pako bila shaka Pa kuvuna shambani,

Kazi niwezayo kufanya Kwa Yesu Mkombozi;

Hivi nikikutegemea, Kwa kuwa wanipenda,

Mapenzi yako nitafanya, Na niwe upendanyo.

2 comments: