Wednesday, November 7, 2012

Nyimbo Za Kikristo No. 1 - 10

Nyimbo Za Kikristo No. 1: Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu
  1. Umtakatifu! Mungu Mwenyezi!Alfajiri sifa zako tutaimba;
    Umtakatifu, Bwana wa huruma, mungu wa vyote hata milele.
  1. Umtakatifu! Na malaikaWengi wengi sana wanakuabudu wote;
    Elfu na maelfu wanakusujudu
    Wa zamani na hata milele.
  1. U mtakatifu! Imgawa gizaLakuficha fahari tusiione,
    U mtakatifu! Wewe peke yako
    Kamili kwa uwezo na pendo.
Nyimbo Za Kikristo No. 2: Twamsifu Mungu
  1. Twamsifu mungu mwana wa upendo, aliyetufia na kupaa juu.
                         Aleluya! Usifiwe, aleluya! Amin; aleluya usiwe, utubariki.
  1. Twamsifu mungu, roho mtukufu,Akatufunulia mwokozi wetu.
  1. Twamsifu mwana, aliyetufia,Akatukomboa na kutuongoza.
  1. Twamsifu mungu, wa neema yote,Aliyetwaa dhambi, akazifuta.
  1. Tuamshe tena, tujaze na pendo.Moyoni uwashe moto wa roho.
Nyimbo Za Kikristo No. 3: Mungu Atukuzwe
  1. Mungu atukuzwe, kwa mambo makuu,Upendo wake ulitupa yesu,
    Aliyejitoa maisha yake,
    Tuwe nao uzima wa milele.
Msifu, msifu dunia sikia;
Msifu, msifu, watuwafurahi;
Na uje kwa baba, kwa yesu mwana
Ukamtukuze kwa mambo yote.
  1. Wokovu kamili zawadi kwetu,Ahadi ya mungu kwa ulimwengu;
    Wanaomwamini na kuungama,
    Mara moja wele husamehewa.
  1. Alitufundisha mambo makuu,Alihakikisha wokovu wetu;
    Lakini zaidi ajabu kubwa,
    Yesu atakuja na tutamwona.
Nyimbo Za Kikristo No. 4: Jina la Yesu, Salamu
  1. Jina la Yesu, salamu! Lisujudieni,Ninyi mbinguni hukumu, Na enzi mpeni.
    Ninyi mbinguni hukumu, Na enzi mpeni.
  1. Enzi na apewe kenu, watetea dini;Mkuzeni bwana wenu, Na enzi mpeni.
    Mkuzeni bwana wenu, Na enzi mpeni.
  1. Enyi mbegu ya rehema nanyi msifuni;Mmeponya kwa neema, Na enzi mpeni.
    Mmeponya kwa neema, Na enzi mpeni.
  1. Wenye dhambi kumbukeni ya msalabani.Kwa furaha msifuni, Na enzi mpeni.
    Kwa furaha msifuni, Na enzi mpeni.
  1. Kila mtu duniani msujudieni,Kote-kote msifuni, Na enzi mpeni.
    Kote-kote msifuni, Na enzi mpeni.
  1. Sisi na wao pamoja tu mumo sifani.Milele sifa ni moja, ni 'enzi mpeni'.
    Milele sifa ni moja, ni 'enzi mpeni.'
Nyimbo Za Kikristo No. 5: Na Tumwabudu Mfalme Mtukufu
  1. Natumwabudu huyo Mfalme,Sifa za nguvu zake zivume;
    Ni ngao ni ngome Yeye milele,
    Ndizo sifa zake kale na kale.
  1. Tazameni ulimwengu huu,Uliyoumbwa ajabu kuu;
    Sasa umewekwa pahali pake,
    Hata utimize majira yake.
  1. Kwa ulinzi wako kwetu Bwana,Twakushukuru U mwema sana;
    Hupewa chakula kila kiumbe,
    Kila kitu kina mahali pake.
  1. Wanadamu tu wanyonge sana,Twakutumaini Wewe Bwana;
    Kamwe haupungui wako wema,
    Mkombozi wetu Rafiki mwema.
Nyimbo Za Kikristo No. 6: Kumekucha Kwa Uzuri
  1. Kumekucha kwa uzuri. Nafumbua macho;Baba amenihifadhi, Ni wake mtoto.
  1. Bwana ni leo kutwa Ulinzini mwako;Nisamehe dhambi niwe Mikononi mwako.
  1. Roho wako anikae Moyoni daima;Anitakase nione Uso wako mwema.
Nyimbo Za Kikristo No. 7: Mungu Msaada Wetu
  1. Mungu Msaada wetu tangu miaka yote,Ndiwe tumaini letu la zamani zote.
  1. Kivuli cha kiti chako ndiyo ngome yetu,Watosha mkono wako ni ulinzi wetu.
  1. Kwanza havijakuwako nchi na milima,Ndiwe Mungu; chini yako twakaa salama.
  1. Na miaka elfu ni kama siku moja kwako,Utatulinda daima. tu wenyeji wako.
  1. Bwana msaada wetu tangu miaka yote,Mlinzi wetu na ngome, daima, milele.
Nyimbo Za Kikristo No. 8:Uje Mkombozi

  1. Unikie ninapolia, Uje M-kombozi;Moyo wangu wakutazamia, Uje M-kombozi.
Nimepotea mbali na kwangu, Nimetanga peke yangu;
Unichukulie sasa kwako: Uje M-kombozi.
  1. Sina pahali pa kupumzika, Uje M-kombozi;Unipe raha, nuru, uzima. Uje M-kombozi.
  1. Nimechoka njia ni ndefu, Uje M-kombozi;Macho yako kuona nataka, Uje M-kombozi.
  1. Bwana daima hutanidharau, Uje M-kombozikilio;Changu utanijibu, Uje M-kombozi.
Nyimbo Za Kikristo No.9: Mwumbaji, Mfalme
  1. Mwumbaji, MfalmeVitu vyote vyako;
    Ni kwa ukarimu wako
    Ninabarikiwa,
    Ni kwa ukarimu wako
    Ninabarikiwa.
  1. Uliyeniumba,Nakutegemea;
    Sina budi kuzisifu
    Hisani zako kuu,
    Sina budi kuzisifu
    Hisani zako kuu.
  1. Nitatoa nini?Kwanza vitu vyote vyako.
    Upendo wako wadai
    Moyo wa shukrani,
    Moyo wako wadai
    Moyo wa shukrani.
  1. Nipewe neema,Niwe nauwezo
    Wa kuishi kwako, Bwana:
    Siku zangu, zako,
    Wa kuishi kwako, Bwana:
    Siku zangu zako.
Nyimbo Za Kikristo No 10: Kristo Wa Neema Yote 
  1. Kristo wa neema yote imbisha moyo wanguMifulizo yabaraka inaamsha shangwe kuu.
    Unifunze nikupende, nikuandame kote,
    Moyo wangu ukajae furaha natumai.
  1. Namshukuru sana Bwana, aniwezesha huku.Salama aniongoza hata kule nyumbani.
    Yesu alinitafuta njiani mbali kwake,
    Akatoa damu yake nipone hatarini.
  1. Kweli mimi mwiwa mkubwa wa neema daima;Wema wako unifunge zaidi kwako Bwana,
    Ili nisivutwe tena kukuacha ee Mponya,
    Nitwalie moyo wangu uwe wako kamili.


8 comments: