Wednesday, November 7, 2012

Nyimbo Za Kikristo No. 11 - 20

Nyimbo Za Kikristo No. 11: Jina La Bwana Li Heri
1. Sauti zote ziimbe, jina la Yesu li heri!
Sifa za mfalme mungu, jina la Yesu li heri!
Jina li heri jina liheri, jina la Yesu li heri!
Jina li heri jina li heri jina la Yesu li heri!
2. Hofu zote latuliza jina la Yesu li heri!
Mwenye dhambi hukubali jina la Yesu li heri!

3. Huvunja nguvu za dhambi, jina la Yesu li heri!
Damu yake hutakasa, jina la Yesu li heri!

4. Sauti yake nitamu, jina la Yesu li heri!
Wakaburini husikia, jina la Yesu li heri!

5. Lugha maelf(u) zitaimba, jina la Yesu li heri!
Astahili mwana-kondoo, jina la Yesu li heri!

Nyimbo Za Kikristo No. 12: Msifu Mungu

1. Msifu Mungu wa neema,
Enyi viumbe po pote;
Wa juu pia sifuni Baba,
Mwana naye Roho! [AMIN]

Nyimbo Za Kikristo No. 13: Yesu Uje Kwetu

1. Umetuahidi ya kwamba wawili Watatu, kwa jina lako wakija,
Utawabariki kwa hivi leo Twapiga magoti nyumbani pako.
Yesu uje kwetu Utubariki,
Yesu uje kwetu Uwe karibu.
2. Umekuwa nasi siku nyingine Tunakuhitaji mpaka mwisho.
Uje Mkombozi; tupe neema; 'Tusikie yesu utubariki.

3. Uje utawale sauti zetu: Nyimbo, nazo sala uzingize.
Imani izidi, ikamilike; Pendo liwe safi, na njia nuru.

Nyimbo Za Kikristo No. 14: Nitembee Nawe

1. Nitembee nawe Mungu
Alivyotembea Henok;
Mkono wangu uushike;
Unene nami kwa pole;
Ingawa njia siioni,
Yesu nitembee nawe.

2. Siwezi tembea peke;
Pana dhoruba mbinguni;
Mitego ya miguu, elfu;
Adui wengi hufichwa;
Uitulize bahari,
Yesu nitembee nawe.

3. Ukinishika mkono,
Anasa kwangu hasara;
Kwa nguvu nitasafiri;
'Tautwika msalaba;
Hata mji wa sayuni
Yesu nitembee nawe.

Nyimbo Za Kikristo No. 15: Nena Mungu

1. Nena rohoni yesu, Nena kwa upole
Sema kwangu kwa pendo, "Huachwi upweke."
'Fungua moyo wangu, Nisikie mara;
Jaza roho na sifa, Sifa zako Bwana.
Kila siku unene, Vile kwa upole,
Nong'oneza kwa pole wa pendo:
"Daima utashinda, Uhuru niwako."
Nisikie maneno: "Huachwi upweke."
2. Nena kwa wana wako, Waonyeshe njia,
Wajaze kwa furaha, Fundisha kuomba;
Wajifunze kutoa Maisha kamili,
Wahimize ufalme, Tumwone Mwokozi.

3. Nena kama zamani, Ulipoitoa
Sheria takatifu: Niiweke pia;
Nipate kutukuza Wewe Mungu wangu,
Mpanzi yako tena, Daima 'kusifu.

Nyimbo Za Kikristo No. 16: Ninakuhitaji

1. Bwana ninakuhitaji! Ni mpofu, maskini;
Unishike mkononi, Kwako napata nguvu.
        Kila saa, Kila saa Bwana ninakuhitaji;
        Kila saa, Kila saa, Unilinde kila saa.
2. Univute na mavazi Ya usikivu wako;
Nguo zangu ni machafu, Nazitamani zako.

3. Wewe ukiniongoza Nitakwenda salama;
Nenda nani siku zote, U nuru na uzima.

4. Na ikiwa m-beleni Sehemu yangu ngumu,
Au ikiwa furaha, Unilinde kila saa.

Nyimbo Za Kikristo No. 17: Si Mimi, Kristo

1. Si mimi, Kristo astahili sifa;
Si mimi, Kristo ajulikane;
Si mimi, Kristo katika maneno,
Si mimi, Kristo kwakila tendo.

2. Si mimi, Kristo, kuponya huzuni;
Kristo pekee, kufuta machozi;
Si mimi, Kristo, kubeba mzigo;
Si mimi, Kristo, kupunga hofu.

3. Kristo pekee, pasipo kujisifu;
Kristo pekee, na nizungunze,
Kristo pekee, na hakuna kiburi;
Kristo pekee, sifa yangu ife.

4. Kristo pekee, mahitaji atoe
Si mimi, Kristo, kisima changu;
Kristo pekee, kwa mwili na kwa moyo;
Si mimi, Kristo, hata milele.

Nyimbo Za Kikristo No. 18: Mwokozi, Kama Mchunga

1. Mwokozi kama mchunga
Utuongoze leo;
Ututume malishoni;
Fanya tayari boma.
Bwana Yesu, peke yako
Umetuvuta kwako.

2. Tu wako, uwe rafiki,
Uwe mlinzi wetu;
Kundi lako ulilinde,
Tusivutwe na dhambi;
Bwana Yesu tusikie,
Tukiomba, samehe.

3. Umetuahidi kwamba
Utakubali watu,
Utawahurumia na
Utawapa neema;
Bwana Yesu, tunapenda
Kuwa, mapema.

Nyimbo Za Kikristo No. 19: Msalabani Pa Mwokozi

1. Msalabani pa Mwokozi Hapo niliomba upozi,
Moyo wangu ulitakaswa, Na asifiwe.
Na asifiwe, na asifiwe.
Alitukomboa kwa damu, Na asifiwe.
2. Chini ya mti msumbufu Niliomba utakatifu,
Alinikomboa kwa damu, Na asifiwe.

3. Kwa ajabu ninaokoka, Yesu anakaa moyoni;
Mtini alinifilia, Na asifiwe.

4. Damu ya Yesu ya thamani Huniokoa makosani;
Huniendesha wokovuni, Na asifiwe.

Nyimbo Za Kikristo No. 20: Mungu Wetu Yeye Mwamba

1. Mungu wetu yeye mwamba, Kimbilio taabuni;
Msaada penye shida ulio karibu sana.
Mwamba wetu kutupumzisha, yu kivuli kuburudusha
Yu mwongozi katika njia, kimbilio taabuni.
2. Mchana usiku, yule kimbilio taabuni,
Hivyo hatutaogopa, kwani yu karibu sana.

3. Iwayo yote, Yeye tu kimbilio taabuni,
Twajua Yeye Mlinzi aliye karibu sana.

4. Mungu wetu Ficho kwetu, kimbilio taabuni.
Siku zote uwe Boma lililo karibu sana.

1 comment: