Nyimbo Za Kikristo No. 21: Baba Twakujia
- Bwana twakujia, Uwe msaada; Uwe kimbilio, twakusihi.
Dunia ni giza tukitengwa nawe;
Tufariji hapa, baba yetu.
Baba teakujia, tu dhaifu, usitugeue, tusikie.
- Salama tulinde, kati ya taabu; Uwe raha yetu mashakani.
Roho yasumbuka, Baba tujalie;
Twakuomba sana, tupe nguvu.
- Neema utupe, tukubali kwako; Moyo wetulinda, safarini;
Tuongoe mbele, tupate kushinda
Na kufika ng'ambo, kule kwako.
Nyimbo Za Kikristo No. 22:
- Usinipite, Mwokozi, unisikie; Unapozuru wengine, usinipite.
Bwana, Bwana unisikie;Unapozuru wengini, usinipite.
- Kiti chako cha rehema, nakitazama; Magoti napiga pale, nisamehewe.
- Sina ya kutegemea, ila wewe tu; Uso wako uwe kwangu: nakuabudu.
- Wewe tu u Mfariji: sina mbinguni, Wala duniani pote, Bwana mwingine.
Nyimbo Za Kikristo No. 23: Yesu Furaha Ya Moyo
- Yesu, furaha ya moyo! Hazina ya pendo, na nuru. Yote yatupendezayo, yasilinganishe nawe.
- Kweli yako ya daima, wawajibu wakwitao, Ni siku zote u mwema kwao wakutafutao,.
- U mkate wa Uzima, kupokea ni baraka, Twanya kwako u kisima roho zikiburudika.
- Mwokozi twakutamani, kwako roho hutulia; Twakushika kwa imani, nawe watubarikia.
- Yesu, ndiwe kwetu mwanga, tufurahishe daima; Giza ya dhambi fukuza, uwe mwanga wa Uzima.
Nyimbo Za Kikristo No. 24: Jina La Yesu Tamu
- Jina lake Yesu tamu Tukilisikia, Hutupoza, tena hamu Hutuondolea.
- Roho ilioumia Kwalo hutibika, Chakula, njaani pia; Raha, tukichoka.
- Jina hili ni msingi, Ngao, ngome, mwamba, Kwa hili napata ungi, Kwangu ni akiba.
- Yesu, Mchunga, Rafiki, Mwalimu, Kuhani,Mwanzo, mwisho, na amina, mali yangu yote!
- Moyo wangu hauwezi Kukusifu kweli; Ila sifa zangu hizi, Bwana, zikubali.
Nyimbo Za Kikristo No. 25: Taji Mvikeni
- Taji mvikeni. Taji nyingi sana, Kondoo mwake Kitini, Bwana wa mabwana;
Nami tamsifu Alikufa kwangu,
Ni Mfalme mtukufu, Seyidi wa mbingu.
- Taji mvikeni Mwana wa Bikira; Anazovaa kichani Aliteka nyara;
Shilo wa manabii Mchunga wa watu
Shina na tanzu ya Yesu wa Bethliehemu.
- Taji mvikeni Bwana wa Mapenzi; Jeraha zake ni shani Ni vito nya enzi,
Mbingu haina Hata malaika
Awezae kuziona pasipo kushangaa!
- Taji mvikeni Bwana wa Salama; Kote - kote duniani Vita vitakoma;
Nayo enzi yake itaendelea,
Chini ya miguu yake, Maua humea.
Nyimbo Za Kikristo No. 26: Tutokapo Tubariki
- Tutokapo tubariki, Utupe kufurahi; Tuwe na upendo wako, Neema ya kushinda.
Nawe utuburudishe tukisafiri chini.
- Twatoa sifa, shukrani Kwa neno la injili; Matunda yake wokovu Yaonekane kwetu;
Daima tuwe amini Kwa kweli yako, Bwana.
- Siku zetu zikizidi Tuzitoe kwa Yesu; Tuwe na nguvu moyoni Tusichoke njiani;
Hata tutakapoona Utukufu wa Bwana.
Nyimbo Za Kikristo No. 26a: Tupe Amani
- Mungu mtukufu Aliyeumba pepo kuvuma Na radi kali; Toa neema unapotawala, Tupe amani Bwana wa wema.
- Mungu wa neema, Nchi imeacha Amri tukufu Na Neno lako; Hasira zako Zisituharibu, Tupe amani, Bwana wa wema.
- Mwumbaji wa haki, Watu wabaya Wamedharau Utukufu wako; Lakini wema wako Utadumu; Endesha kweli Bwana wa wema.
- Tunakutolea Ibada safi Kwa ajili ya Wokovu wako; Hivi tunaziimba Sifa zako; Wako uwezo Na utukufu.
Nyimbo Za Kikristo No. 27: Tena, Mwokozi, Twalitukuza Jina Lako
- Tena, Mwokozi, twalitukuza Jina lako lenye kupendeza,
Twangojea neno la amani,
Kabla hatujakwenda nyumbani.
- Tupe amani njiani mwetu, Wewe u mwanzo, u mwisho wetu;
Dhambini kamwe isiingie
Midomo ikitajayo wewe.
- Utupe amani usiku huu, Ili gizani kuwe nuru kuu.
Tulinde kwa kuwa kwako Bwana.
Usiku ni sawa na mchana.
- Tupe amani ulimwenguni Ndiyo dawa yetu majonzini;
Na ikitwita sauti yako,
Tupe amani milele kwako.
Nyimbo Za Kikristo No. 28: Jina La Thamani
- Jina lake Yesu tamu, Lihifadhi moyoni; Litatufariji ndugu, Enda nalo po pote. Jina la (Thamani) thamani, (thamani) Tumai la dunia Jina la (Jina la thamani-tamu!) thamani,Furaha ya mbinguni.
- Jina la Yesu lafaa Kama ngao vitani, Majaribu yakisonga, Omba kwa jina hili.
- Jina hili la thamani Linatufurahisha, Anapotukaribisha, Na tunapomwimbia.
- Mwisho wa safari yetu Tutakapomsujudu, Jina hili tutasifu Furaha ya mbinguni.
Nyimbo Za Kikristo No. 29: Yesu, Nakupenda
- Yesu nakupenda, U mali yangu, Anasa za dhambi sitaki kwangu;
Na mwokozi aliyeniokoa
Sasa nakupenda, kuzidi pia.
- Moyo umejaa mapenzi tele Kwa vile ulivyonipenda mbele,
Uhai wako ukanitolea
Sasa nakupenda, kuzidi pia.
- Ulipoangikwa Msalabani Tusamehewe tulio ndambini;
Taji ya miiba uliyoivaa,
Sasa nakupenda, kuzidi pia.
- Mawanda mazuri na masikani Niyatazamapo huko mbinguni,
'Tusema na taji nitakayovaa
Sasa nakupenda, kuzidi pia.
Nyimbo Za Kikristo No. 30: Yesu, Unipendaye
- Yesu unipendaye kwako nakimbilia, Ni wewe utoshaye mwovu akinijia.
Yafiche ubavuni mwako maisha yangu;
Nifishe bandarini, wokoe moyo wangu.
- Ngome nyingine sina; nategemea kwako, Usinitupe Bwana, nipe neema yako,
Ninakuamania, mwenye kuniwezesha;
Shari wanikingia, vitani wanitosha.
- Nakutaka Mpaji, vyote napata kwako; Niwapo muhitaji, utanijazi vyako;
Nao waangukao wanyonge wape nguvu;
Poza wauguao, uongoze vipofu.
- Mwana umeniosha moyo kwa damu yako; Neema ya kutosha yapatikana kwako;
Kwako Bwana naona kisima cha uzima;
Mwangu moyoni, Bwana, bubujika daima.
No comments:
Post a Comment