Monday, November 3, 2014

Nyimbo Za Kikristo: 201-220

201. Hunipenda Pia.
He Loves me, too

1. Mungu huona videge wanaoanguka;
Akiwapenda videge,vile hunipenda.

Hunipenda, hunipenda, pia;
Najua ananipenda niliye mdogo.

2. Rangi ya namna nzuri upamba maua;
Akiyapenda maua, vile unipenda.

3. Mungu aliyeviumba videge, maua,
Atasahau watoto kweli huwapenda.

202. Sikia Mlio
Hear the Pennies Dropping

1. Sikia mlio! Pesa koponi
Zinalialia—zote kwa Yesu.

Kuanguka kuanguka pesa koponi,
Kila moja kwako, Yesu zipokee.

2. Huanguka pesa toka mikononi:
Sadaka kwa Yesu ya kundi dogo.

3. Tulio wadogo tuna haba tu;
Tuishapo kuwa Pendo 'tazidi.

4. Wenye mali chache tumpe moyo;
Kwa furaha tupu atakubali.

203. Ya Saba Ni Kwa Yesu
The Seventh Day Is For Jesus

1. Siku sita fanya kazi, Ya saba ni kwa Yesu.
Hapo tunapo pumzika, kwani ni yake Yesu.

Moja, mbili, tatu,nne, tano, sita, zote kwetu;
Lakini tutakumbuka, Ya saba ni kwa Yesu.

2. Huonyesha ya kufanya, Kwa kuwa ni ya Yesu,
Na atuonyesha njia, tutamfuata Yesu.

3. Tuombe kila Sabato, Na kujifunza kwake;
Tutamtii daima, tutakaa na Yesu.






204. Kuwa Na Yesu Nyumbani
Happy, Happy, Home

1. Kuwa na Yesu nyumbani,
Furaha nyingi,
Furaha nyingi, Furaha nyingi.
Kuwa na Yesu nyumbani,

2. Yesu yu ndani ya Baba,
Nyumba salama, nyumba salama, nyumba salama;
Yesu yu ndani ya Baba.
Nyumba salama, nyumba salama.

3. Yesu yu ndani ya Mama . . .

4. Yesu ndani ya watoto . . . .

205. Msifu Mungu Ee Watoto
Praise Him, Praise Him

1. Msifu Mungu, Ee watoto wote,
Yu pendo, Yu pendo;
Msifu, Msifu, Ee watoto wote
Mungu ni upendo.

2. Tunampenda, Ee watoto wote,
Yu pendo, Yu pendo,
Tunampenda, Ee watoto wote
Mungu ni upendo.

3. Timikeni, Ee watoto wote.
Yu pendo, Yu pendo,
Tumikeni, Ee watoto wote
Mungu ni upendo.

206. Mwokozi Wangu Anipenda
Now I Belong To Jesus

1. Mwokozi wangu alinipenda,
Maovu ayanitengi naye,
Alijitoa, kuniponya,
Sasa mimi wake.

Mimi wake kabisa,
Naye Yesu wangu,
Si kwa wakati huu tu,
Bali na milele.

2. Dhambi nilijidhili sana,
Yesu akaja kunikomboa,
Akanitoa sumbukoni,
Sasa mimi wake.

3. Furaha nyingi moyoni mwangu,
Bwana Yesu kunifanya huru,
Kunitwaa kwa damu yake,
Sasa mimi wake.

207. Nani Afanya Maua
Who Makes The Flowers

1. Nani ayafanya maua, maua,
Nani ayafanya—Mungu juu.

2. Nani apambaye machweo, machweo,
Nani ayapamba—Ni Mungu.

3. Nani afanya theluji, theluji,
Nani aifanya—ni Mungu.

208. Mungu Afanya Upinde
The Rainbow

1. Nani afanya upindi,
Namjua, namjua
Mungu afanya upindi
Nampenda kwa hiyo.

2. Mungu atuma upindi
Ni bora mweupe,
Mungu atuma upindi,
Kwamba yu karibu.

209. Napenda Sana Kifika
I Love to Come to Sabbath School

1. Napenda sana kufika, skuli ya Sabato
Napenda sana kufika, siku ya Sabato

2. Napenda sana kuimba, habari za Yesu,
Napenda sana kuimba, siku ya Sabato.

3. Napenda sana kutoa, sadaka kwa Yesu,
Napenda sana kutoa, siku ya Sabato.

4. Napenda sana kuomba kwa Yesu, kwa Yesu,
Napenda sana kuomba, siku ya Sabato.

5. Napenda sana kujua, maneno ya Yesu,
Napenda sana kujua, siku ya Sabato.

6. Napenda sana kusema, Fungu la kukariri,
Napenda sana kusema, Siku ya Sabato.

210. MAITIKIO
Roho Wa Mungu Wangu
Spirit of the Living God

Roho wa Mungu wangu, Nakuhitaji!
Roho wa Mungu wangu, Nakuhitaji!
Unilinde na unijaze;
Roho wa Mungu wangu, Nakuhitaji!

211. Moyoni
(Into My Heart)

Moyoni, moyoni; Ingia moyoni, Yesu.
Njoo leo, njoo kukaa, Ingia moyoni Bwana.
Moyoni, moyoni, Angaza moyoni Yesu,
Ng'aa leo siku zote, Angaza moyoni Bwana.

212. Mtazame Mwokozi
(Turn Your Eyes Upon Jesus)

Mtazame Mwokozi,
Usoni Mwake mzuri,
Mambo ya dunia hugeuka,
Usowake tukiuona.

213. Niwe Nao Uzuri Wa Mwokozi
(Let the Beauty of Jesus)

Niwe nao uzuri wa Mwokozi,
Nazo huruma Zake na usafi,
Roho Mtakatifu anibadilishe,
Aonekane Yesu ndani yangu.

214. Nataka Niwe Tayari
(I Want to be Ready When Jesus Comes)

Nataka niwe tayari, Bwana,
Nataka niwe tayari, Bwana,
Furaha za ulimwengu ni bure;
Nilinde hata uje!

215. Ulimwengu Wataka
(What the World Needs is Jesus)

Ulimwengu wataka kumwona Yesu;
Ulimwengu wataka kumwona Yesu.
Analeta furaha, shangilio kutosha,
Ulimwengu wataka kumwona Yesu.

216. Moyoni 'Nijaze
(With Thy Spirit Fill Me)

Moyoni 'nijaze,
Na Roho wa Yesu;
Nataka kujitoa,
Moyoni 'nijaze.

217. Omba Sana Asubuhi
(Whisper a Prayer in the Morning)

Omba sana asubuhi,
Omba sana mchana,
Omba sana na jioni,
Bwana hutusikia.

Mungu hujibu maombi,
Asubuhi na mchana,
Hata hutungojea tena,
Wakati wa jioni.

Na tuimbe asubuhi.
Tena saa za mchana.
Hivi tutafurahi Naye.
Pumziko la jioni.

218. Yesu Mwokozi Mpendwa
(Wonderful, Wonderful Jesus)

Yesu Mwokozi Mpendwa.
Hakuna mwingine!
Yesu Mwokozi Mpendwa,
Yesu Mwokozi Mpendwa,
Nakutazama wewe pekee,
Yesu Mwokozi Mpendwa,
Ninakutafuta;
Wewe u mali yangu.
Sasa na milele.

219. Pambazuka Nuru
(There's a New Day Dawning)

Pambazuka nuru,
Siku mpya yaja,
Basi amkeni na kuimba,
Ninyi nyote!
Pambazuka nuru,
Siku mpya yaja,
Yesu atakaporudi kama Mfalme!

220. Kwa Heri
(Goodbye Chorus)

Kwa heri, Mungu awalinde;
Kwa heri, na awaongoze;
Kwa heri, na kuwapa amani,
Bwana awabariki.

Nyimbo Za Kikristo: 161-180

161. Piga Panda
Lift Up The Trumpet

1. Piga panda na ya makelele; Yesu yuaja tena!
Ipate sauti, imba sana; Yesu yuaja tena!

Anakuja, anakuja; Yesu yuaja tena!

2. Itoe mwangi sana vilima; Yesu yuaja tena!
Yuaja kwa utukufu mwingi, Yesu yuaja tena!

3. Itangazwe mahali po pote; Yesu yuaja tena!
Mwokozi aliye tufilia, Yesu yuaja tena!

4. Kuona machafuko twajua Yesu yuaja tena!
Mataifa ya kasiriana, Yesu yuaja tena!

5. Maradhi, hofu hutuhubiri Yesu yuaja tena!
Taabu, njaa hutulilia Yesu yuaja tena!

162. Tumaini Liko
There Is a Blessed Hope

1. Tumaini liko La thamani kuu,
Kupita anasa tupu zake ulimwengu.

2. Pana nyota nzuri: Nuru itoayo
Kwetu wakati wa kifo Ndio ufufuo.

3. Zikiumwa roho Na hofu, mashaka,
Sauti hutuambia Mungu hutupenda.

4. Kutoka Kalwari Sauti hunena;
Nyota ni nuru ya mbingu, Tumaini letu.

















163. Anakuja, Bwana Yesu
It May Be A Morn

1. Pengine ni saa ya kupambazuka, Mishale ya jua ipenyapo giza,
Kwamba atakuja Yesu mtukufu, Awapokee wake.

Bwana itakuwa lini Tutapoimba
"Anakuja, Bwana Yesu, Aleluya, Amin, Aleluya, Amin?"

2. Pengine mchana, pengine jioni, Pengine usiku wa manane, giza
Itatoweka kwa fahari akija, Awapokee wake.

3. Majeshi yake yataimba "Hosana," Na watakatifu waliotukuzwa
Watamsifu kwa kuwa amekuja Awapokee wake.

4. Furaha tukiitwa pasipo kufa, Pasipo kuona maradhi, machozi;
Kuchukuliwa winguni kwa fahari Akija kwa watu wake.

164. Mishale Ya Nuru
The Golden Mornig

1. Unakaribia wakati wa Kuja kwa Yesu.
Atawachukua watu wake Nyumbani juu.

Tunaiona mishale ya nuru Inayopenya giza;
Tunaiona mishale ya nuru Ya ufunuo.

2. Injili inatangazwa pote kwa mataifa;
Bwana wa Arusi atakuja Na tarumbeta.

3. Pamoja na malaika zake Bwana arudi,
Awapeleke waaminifu Wasife tena.

4. Wapenzi waliotengwa kale Watakutana;
Machozi yao wenye huzuni Yatafutika.

165. "Uwe Imara"
Sweet Promise Is Given

1. Ahadi tamu kwa waamini, Tazama nakuja upesi sana.
Uwe imara, hatari kubwa: Ndugu usilale, bali ukeshe.

Uihifadhi imani yako,--Dunia mpya itatolewa
Njoo ingia furaha yangu; Taji zinangoja; Uwe imara.

2. Tatakesha na kutoa sala; Atakuja kama mwivi kwa wengi;
Ya kwamba yu karibu twajua, Ila hatujui ni siku gani.

3. Tunategemea Neno lake, Ambalo latangaza kuja kwake,
Tumaini letu ni ahadi: "naja karibuni, uwe imara."

166. Furaha Kwa Ulimwengu
Joy to the World
1. Furaha kwa ulimwengu, Bwana atakuja!
Kila moyo umpokee, Viumbe imbeni,
Viumbe imbeni, Viumbe vyote imbeni.

2. Na Bwana atatawala: Watu na waimbe;
Mit, milima na mawe Kariri furaha,
Kariri furaha, Kariri furaha kubwa.

3. Atatawala kwa wema; Atawafundisha
Mataifa haki yake, Ajabu za pendo,
Ajabu za pendo, Ajabu za pendo lake.

167. Yu Hai, Yu Hai
(He Lives, He Lives)

1. Yesu Bwana Mwokozi aishi milele,
Najua kwamba Yupo pamoja na mimi;
Sauti nasikia, Rehema naona;
Wakati namhitaji, yupo nami.

Yu hai, Yu hai,Yu hai Bwana Yesu!
Atembea, azungumza nami siku zote.
Yu hai, Yu hai, kutoa uzima!
Hivi ndivyo nijuavyo,
Yu hai ndani yangu!

2. Ulinzi Wake upo naona dhahiri,
Miguu ichokapo, sikati tamaa.
Najua an'ongoza kupota dhoruba,
Siku ya kuja kwake nitamwona.

168. Tarumbeta Ya Mwana
Wahen the Trumpet of the Lord

1. Tarumbeta ya mwana itakapolia mara,
Milele itakapopambazuka,
Nao wa haki watakapokusanyika ng'ambo,
Majina yaitwapo, lo!—niweko.

Majina yaitwapo, lo!—
Majina yaitwapo, lo!—
Majina yaitwapo, lo!—
Majina yaitwapo, lo!—niweko.

2. Siku ile watakatifu watakapoamka
Na kuondoka huru kaburini
Watakapokusanyika makaoni kule juu,
Majina yaitwapo, lo—niweko.

3. Tutende kazi kwa yesu mchana kutwa kwa bidii,
Tutangaze kote pendo lake kuu,
Nayo kazi itakapotimika hap chini
Majina yaitwapo, lo—niweko.

169. Tutashindae Hukumuni?
When Jesus Shall Gather

1. Hapo Yesu atakapoita mataifa mbele yake,
Tutashindaje kwenye hukumu mbele ya kiti cha enzi?

Atakusanya ngano ghalani, atatupambali makapo;
Tutashindaje hukumuni siku kuu ya kiyama?

2. Je, tutasikua neno tamu: "vema, wewe mtumwa mwema,"
Ama wenye uchunguna hofu tutakatazwa ufalme?

3. Atakubali tu kwa furaha watoto wake wapendwa,
Atawapa mavazi meupe, wakea tayari kumlaki.

4. Hivyo tukeshe, nasi tungoje, wenye taa zinazo waka;
Tutakapoitwa arusini tuwe tayari kumlaki.

5. Roho ikielekea mbingu twangoja wenye saburi,
Hata safari yetu iishe, tukae kwake milele.

170. Jina Langu Limeandikwa Je?
Lord, I Care not for Riches

1. Siitafuti mali, wala utajiri;
Nataka kwa yakini nipate Mwokozi.
Chuoni mwa Ufalme, niambie Yesu,
Jina langu yakini limeandikwa, Je?

Limeandikwa, Je? Jina langu huko?
Kitabuni mbinguni, limeandikwa je?

2. Dhambi zangu ni nyingi, ni kama mchanga,
Lakini damu yako, Mwokozi, Yatosha;
Kwani umeahidi: zijapo nyekundu
Zitakuwa nyeupe ilivyo theluji.

3. Mji mzuri sana, wa majumba makuu,
Walipo malaika, mji bila ovu;
Wakakapo walio na mavazi safi,
Limeandikwa sasa, jina langu huko?

171. Hukumu
The Judgment Has Set

1. Imeanzishwa hukumu mbinguni; Tutasimamaje pale
Apomapo Mungu hakimu kula wazo na tendo?

Tutasimamaje sote katika siku kuu ile?
Dhambi zitu zitafutika ama zitatuangusha?

2. Wametangulia wafu kupimwa, Kitambo ndipo wahai,
Watapokea neno la mwisho, Vitabuni mwa Mungu.

3. Tutasimamaje usiku ule, Siri zetu, kila moja,
Zafunuliwa toka vitabu; Yesu atusaidie!

172. Mfalme Ajapo
Called To The Feast

1. Mfalme wetu atuita tukae karamuni kwake;
Itakuwaje nasi kule Bwana akija?

Bwana ajapo, ndugu, Bwana ajapo!
Itakuwaje na sisi, Bwana akija?

2. Atavikwa vizuri sana,taji badala ya miiba;
Kweli tokeo la fahari Bwana ajapo.

3. Kwa fufaha awakubali wenye mavazi ya arusi;
Tu wa heri tukimridhisha Bwana ajapo.

4. Kutakuwako na utengo: watalia waliomwasi;
Cha kutisha kitambo kile Kristo ajapo!

5. Mfalme utupe neema sisi tunapokungojea
Tusiogope kukuona ujapo Bwana.
173. Hatujui Saa
We Know Not the Hour

1. Hatujui sa-a ya kuja kwwa Bwana, Lakini dakiki zasema karibu
Atakporudi,--lakini kwa kweli Hatujui sa-a.

Atakuja, kwa vile tukeshe;
Atakuja Mwokozi, Aleluya!
Atakuja kwa fahari yu Baba yake,--
Hatujui sa-a.

2. Pana nuru kwao wapendao haki, pana kweli katika chuo cha Mungu;
Unabii hufundisha kuja kwake,--Hatujui saa.

3. Tutakesha na tutaomba daima, Tutafanya kazi mpaka akija,
Tutaimba na tutasoma ishara,--Hatujui saa.

174. Tukimngojea
We Know not the Time when He Cometh

1. Sijui atakapokuja, 2. Nakumbuka huruma zake,
Mchana au usiku; Bei ya wokovu wetu:
Labda sa-a ya alasiri, Aliacha nyumba tukufu
Pengine ni alfajiri. Awafilie wabaya.
Hutwambia tuwe tayari, Ninadhani itampendeza,
Ta-a zetu tusizime; Kama sisi watu wake,
Ili ajapo atukute; Tukionyesha pendo letu,
Tuwe tukimngoja Yeye. Tuwe tukimngoja Yeye

Tu - - - kimngojea - - - a, 3. Ee Yesu, Mwokozi mpendwa,
(kukesha, tunakungoja Wewe) Wajua nalihifadhi
Tu - - - kimngojea - - - a, Tumaini la kukuona.
(kukesha, tunakungoja Wewe) La kukaribishwa nawe
Tu - - - kimngojea - - - a, Ukija kwa watu wengine,
(kukesha, tunakungoja Wewe) Kama mhukumu wao,
Twakesha, twamngoja Yeye. Kwangu utakuwa rafiki,--

Nakesha, nakungojea.

175. Uso Kwa Uso
Face to Face

1. Nitaonana na Yesu, uso kwa uso kweli;
Siku ile shangwe tele nitamwona Mwokozi.

Tutaonana kwa macho, huko kwetu mbinguni;
Na kwa utukufu wake, nitamwona milele.

2. Sasa siwezi kujua jinso alivyo hasa,
Bali atakapokuja, nitamwona halisi.

3. Mbele yake yafukuzwa machozi na huzuni;
Kipotovu kitanyoshwa, fumbo litafumbuka.

4. Uso kwa uso! Hakika palepale furaha;
Nitafurahi kabisa nikimwona Mwokozi.

176. Ati Tuonane Mtoni?
Shall we Gather at River

1. Ati twonane mtoni? maji mazuri ya mbingu;
Yanatokea mwangani, penye kiti cha Mungu.

Naam, twonane mtoni! Watakatifu, kwenu ni mtoni!
Tutakutanika kule mtoni penye kiti cha Mungu.

2. Tukitembea mtoni na Yesu mchunga wetu,
Daima tu ibadani usoni pake kwetu.

3. Tukisafiri mtoni tutue ulemeao,
Wema wa Mungu yakini: una taji na vao!

4. Kwang'ara sana mtoni cha Mwokozi ni kioo,
Milele hatuachani tumsifu kwa nyimbo.

5. Karibu sana mtoni, karibu tuatawasili,
Mara huwa furahani na amani ya kweli.

177. Kazi Yangu Ikiisha
When my Life-work is Ended

1. Kazi yangu ikisha, nami, nakiokoka,
Na kuvaa kutokuharibika,
Nitamjua Mwokozi; nivukapo ng'amboni
Atakuwa wa kwanza kunilaki.

Nitamjua, nitamjua,
Nikimwona uso kwa uso;
Nitamjua, nitamjua,
Kwa alama za misumari.

2. Kuona uso wake utanipa furaha,
Furaha isiyo ya kukomesha;
Nitamsifu Mwokozi kwa rehema na pendo
Vilivyo nipa pahali mbingini.

3. Nao walio kufa katika Bwana Yesu,
Nitawaona tena huko juu;
Lakini nifikapo kwake huko mbinguni,
Nataka kumwona Mwokozi kwanza.

4. Milangoni mwa mji Bwana atanipisha,
Pasipo machozi awla huzuni.
Nitauimba wimbo wa milele: lakini
Nataka kumwona Mwokozi kwanza.




178. Ukingoni Mwa Yordani
On Jordan's Stormy Banks

1. Ukingoni mwa Yordani ninaangalia
Bara nzuri ya Kaanani, ninayotamani.

Tutakaa pamoja na Yesu,
Katika pwani yenye raha;
Tutaimba wimbo wa Musa na Kondoo,
Milele hata milele.

2. Bara ile ina nuru, nuru ya milele;
Kristo, Jua, hutawala, hufukuza giza.

3. Nitapafikia lini na kubarikiwa,
Penye ufalme wa Baba. Na kumwona uso?

4. Furaha yangu rohoni ni kuchukuliwa;
Siyaogopi mawimbi katika Yordani.

179. Watafurahi
O There'll Be Joy

1. Wavunaji watafurahi, pale watakapo rudi,
Wakiyaleta mavuno hata Yerusalemu.

Furaha wataipata, furaha hata milele,
Furaha, wataipata, wakati wa mavuno.

2. Na siku ile tutaimba, kumshukuru na kumsifu
Bwana Yesu Jumbe wetu, kule Yerusalemu.

3. Wavunaji watafurahi makaoni mwa milele
Yaliyowekwa tayari kule Yerusalemi.

180. Pana Mahali Pazuri Mno
There's a Land

1. Pana mahali pazuri mno,
Twapaona kwa mbali sasa;
Baba yetu angoja pale,
Amepanga makao yetu.

Kitambo tu bado,
Tutakutana ng'ambo pale.
Kitambo tu bado,
Tutakutana ng'ambo pale.

2. Tutaimba pale kwa moyo
Nyimbo tamu za wenye heri.
Na rohoni hatutaona
Tena haja ya kupumzika.

3. Kwa Baba yetu mkarimu
Tutatoa shukrani sana,
Kwa kipaji cha pendo lake
Na baraka anazotupa.

Nyimbo Za Kikristo: 141-160

141. Chini Ya Msalaba
Beneath the Cross of Jesus

1. Chini ya msalaba Nataka simama;
Ndio mwamba safarini, Wa kivuli chema;
Ni kweli kwa roho yangu Ni tuo kamili,
Tatua mziho wangu Wakati wa hari.

2. Hapa ni pema sana, Ni ngome kamili;
Hapa yameonekana, Mapenzi ya kweli;
Kama alivyoonyeshwa Yakobo zamani,
Msalaba umekuwa ngazi ya mbinguni.

3. Na Yesu Msalabani Walimkimea,
Alikufa niokoke Niliyepotea:
Naona ajabu sana Ya manbo mawili
Jinsi alivyonipenda Nisiyestahili.

4. Atakayeonana Na Yesu mbinguni,
Njia yake aanzapo Ni Msalabani;
Wokovu upo hapa tu, Mwingine hapana,
Kisha kuna furaha kuu Pamoja na Bwana.
142. Nasikia Sauti Yako
I hear Thy Welcome Voice

1. Nasikia mwito, Ni sauti yako;
Nikasafiwe kwa damu Ya kwangikwa kwako.

Nimesongea mtini pako,
Unisafi kwa damu ya kwangikwa kwako.

2. Ni mnyonge kweli, umenipa nguvu;
Ulivyonisfi taka Ni utimilivu.

3. Yesu hunijuvya: Mapenzi imani,
Tumai, amani, rahi, hapa na mbinguni.

4. Napata wokovu, Wema na neema;
Kwako Bwana nina nguvu Na haki daima.





143. Naamini
Father, I Stretch My Hands

1. Baba sina msaada ila kwako pekee;
Kama kwangu ungefichwa, Nifanyeji, Baba?

Sasa hivi naamini Yesu alikufa,
Aliimwaga damu yake, Nitoke dhambini.

2. Naamini mwana wako Nipe nguvu zako;
Nijazie mahitaji, katika saa hii.

3. Nifuraha gain kwangu kukuona uso!
Nijue sauti yako, Nipate neema.

144. Ni Wako Bwana
I am Thine O Lord

1. Ni wako Bwana, ninasikia Unaponena nami;
Lakini, kweli, nataka kwako Nizidi kusongea.

Bwana vuta, (vuta) nije nisongee
Sana kwako mtini.
Bwana, vuta, vuta, nije nisongee
Pa damu ya thamani.

2. Niweke sasa nikatumike kwa nguvu za neema;
Uyapendayo nami nipende Nizidi kukwandama.

3. Nina furaha tele kila saa nizungumzapo nawe;
Ninanena kama kwa rafiki Nikipiga magoti.

145. Namtaka Bwana Yesu
Take The World

1. Ulimwengu siutaki, Namtaka Bwana yesu;
Dunia hunidanganya; yesu yu mwaminifu.

Rehema ni ya ajabu! Pendo bila kipimo!
Wokovu mkamilifu, Amana ya uzima.

2. Ulimwengu siutaki, Namtaka Bwana yesu;
Kati ya dhoruba kali Yeye wimbo mtamu.

3. Ulimwengu siutaki, namtaka Bwana yesu;
Safarini duniani Yeye furaha yangu.

4. Ulimwengu siutaki, Namtaka Bwana yesu;
Msalaba naamini, Hata Namwona Yesu.

146. Twae Wangu Uzima
Take My Life and Let It Be

1. Twae wangu uzima sadaka ya daima;
Twae saa na usiku Zikutukuze huku.

2. Twae mikono nayo, ifanye upendayo,
Twae yangu miguu, Kwa wongozi wako tu.

3. Twae sauti yangu, niimbe kwa Mungu tu;
Itwae na midomo, Ijae neno lako.

4. Twae dhahabu pia Na yote ya dunia;
Twae yangu hekima, upendavyo tumia.

5. Nia itwae, Mungu, haitakuwa yangu;
Twae moyo; ni wako, uwe makazi yako.

6. Twae mapenzi yangu, sifa za moyo wangu;
Twae kabisa nafsi Niwe wako halisi.

147. Uishi Ndani Yangu
Love Out Thy Life Within Me

1. Tawala ndani yangu, Ee Yesu, Mfalme.
Uwe kwangu majibu kwa maswali yangu;
Uishi ndani yangu, Wewe, mwongozi
Utumishi ni wangu, Wako utukufu.

2. Hekalu nimetoa, Umelisafisha;
Sasa fahari yako Imulike ndani;
Dunia iwe kumya, mwili sasa uwe
Mtumwa mtulivu Wa kukutii tu.

3. Viungo vyake mwili, Vyote vikungoja
Tayari vikuutwa Kwenda, kusimama;
Bila manumguniko au malaumu,
Au kusumbuliwa, Pasipo majuto.

4. Niwe na utulivu pasipo haraka;
Tayari kungojea maagizo yako.
Tawala ndani yangu, Ee Yesu, Mfalme,
Uwe kwanfgu majibu kwa maswali yote.

148.Univute Karibu
Closer to Thee, My Father, Draw Me

1. Univute karibu, Baba, Unikumbatie;
Unisogeze kifuani, Nataka pumziko.

Univute karibu(Vuta, univute karibu)
Kwa kamba za upendo, (Kwa kamba, kamba za upendo)

Univute (kwa kamba za upendo, Univute karibu)
Karibu nawe. (Univute karibu)

2. Univute Mwokozi wangu, Na tusiachane;
Mikono yako juu yangu Leo nione.

3. Univute kwa Roho yako, Nifanane nawe;
Unioshe, unihuishe, Niwe safi, huru.

149. Kuwa Wake Yesu
Would You Live for Jesus

1. Kuwa wake Yesu, je! Ni kusudi lako?
Ungeenda naye njia nyembamba?
Unataka aubebe mzigo wako?
Awe Mwongozi wako.

Uwezo wake unakutosha
Na danu yake itakusafi;
Kwa vile ukubali ni bora
Afanye mapenzi yake nawe

2. Unataka kutika unapokwita?
Kupata amani kwa kumpa vyote?
Wataka uwezo usianguke kamwe?
Awe Mwongozi wako.

3. Wataka raha katiak ufalme wake?
Ungeshinda kwa majaribu yote?
Ungefanya kazi yake vizuri sana?
Awe Mwongozi wako.

150. Hasha Maneno Mabaya Yasitoke
Angry Words! Oh, Let them Never

1. Hasha, maneno mabaya yasitoke kinywani
Moyo mwema uzuie Ndimi, zisichafuke.

"Nanyi pendeni", Asema yesu,
(Mpendane) (Mpendane)
Kama mwanzo alivyotupenda:
"Nanyi pendeni", alivyotupenda:
(Mpendane) (Mpendane)
Wana, tiini amri hii. (amri heri hii).

2. Pendo ni mtakatifu; Urafiki; mzuri:
Visiharibike mara kwa kunena vibaya.

3. Tusinene kwa hasira, inazaa huzuni,
Pendo lako ee mwokozi, Inatosha tushindi.

151. Huniongoza Mwokozi
He Leadeth Me

1. Huniongoza Mwokozi, ndipo nami hufurahi,
Niendapo pote napo, ataniongoza papo.

Kuongoza hunishika; kwa mkono wa hakika;
Nitaandamana naye Kristo aniongozae.

2. Pengine ni mashakani nami pengine rahani;
Ni radhi, ijayo yote, yupo nami siku zote.

3. Mkono akinishika kamwe sitanung'unika;
Atakachoniletea ni tayari kupokea.

4. Nikiisha kazi chini sita kimbia mauti;
Kushinda ni ya hakika nikiongozwa na Baba.

152. Karibu Na Wewe, Mungu Wangu
Nearer, My God, to Thee

1. Karibu na wewe, Mungu wangu:
Karibu zaidi Bwana wangu,
Siku zote niwe karibu na Wewe,
Karibu zaidi, Mungu wangu.

2. Mimi nasafiri duniani,
Pa kupumzika sipaoni,
Nilalapo niwe karibu na Wewe,
Karibu zaidi, Mungu wangu.

3. Yote unipayo yanivuta;
Pa kukaribia nitapata;
Na nielekezwe, karibu na Wewe,
Karibu zaidi, Mungu wangu.

4. Na kwa nguvu zangu nikusifu;
Mwamba, uwe maji ya wokovu
Mashakani niwe kaaribu na Wewe;
Karibu zaidi, Mungu wangu.

5. Na nyumbani mwa juu, Baba yangu
Nikinyakuliwa toka huko,
Kwa furaha niwe pamoja na Wewe,
Karibu zaidi, Mungu wangu.




153. Fikira Moja Tu
One Sweetly Solemn Thought

1. Fikira moja tu
Hurejea tena
Nimekaribia mbingu
Zaidi ya jana.

Karibu na kwetu mbingu,
Karibu na kwetu sasa,
Nikwone karibu.

2. Karibu na kwetu
Na kwenye makao;
Kiti cha enzi cha Mungu,
Pahali pa mto.

3. Kamilisha Yesu,
Kuamini kwangu;
Nikifika mwisho wangu,
Nikwone karibu.

154. Yanipasa Kuwa Naye
I Must Have The Saviour With Me

1. Yanipasa kuwa naye, Mwokozi Bwana wangu,
Akiwa karibu nami, napata nguvu kweli.

Moyo hauogopi, wala kitikisika.
Nitakwenda apendapo. Kwa kuwa anilinda.

2. Yanipasa kuwa naye, kwani nategemea;
Anaweza kufariji na maneno matamu.

3. Yanipasa kuwa naye maisha yangu yote;
Yakiwapo majaribu na mashaka yo yote.

4. Yanipasa kuwa naye katika njia zangu;
Macho yake yaongoza hatua zangu zote.

155. Njiani Huniongoza
All the Way my Saviour Leads Me

1. Njiani huniongoza. Yesu wangu, Mwokozi;
Rehema hatapunguza, Milele Kiongozi.
Ina raha kwandamana Duniani daima;
Nijaposumbuka sana, Yeye hutenda vyema,

2. Njiani huniongoza Hupunguza matata;
Nikiugua hupoza, Na njaani nashiba.
Lichokapo guu langu Nguvu zikapungua,
Jiwe lilo mbele yangu Hunibubujikia.

3. Njiani huniongoza Kwa pendo zilizo kuu,
Mwisho atanituliza Kwake Baba yangu juu.
Nikivikwa kutokufa, Nikae na Mwokozi,
Nitamsifu sana; sifa: "Kweli ni Kiongozi."

156. Uniongoze, Yehova
Guide Me, O Thou Great Jehovah

1. Uniongoze, Yehova, Ni msafiri chini;
Ni mnyonge, u hodari, 'Nilinde kwa mkono.
Unitunze, unilinde, Unionyeshe njia!

2. Na kisima cha uzima, Maji ya utabibu,
Fungua kwa moyo wangu, Ninywe na kuponyeka!
Uninyweshe, unilishe, Hata nimetosheka.

3. Wakati wa kuuvuka, Ule mto Yordani,
Hofu yangu ufariji, 'Nione uso wako.
Nyimbo shangwe, nyimbo shangwe, Nitaimba daima.

157. Mfalme Yu Mlangoni
The Coming King

1. Mfalme yu mlangoni, Ndiye aliyetufia;
Mara wote wampendao atawakusanya.

Yuaja, yuaja, mlangoni anasimama;
Anakuja, anakuja, Kuja kwake karibu.

2. Dalili za kuja kwake Zinazidi kutimizwa;
Karibu wateule watamlaki Bwana.

3. 'Sitafute duniani amani wala furaha,
Mpaka Bwana arudi dhambi kuondoa.

4. Tutakaa na Mwokozi Makaoni ya milele;
Daima tutafurahi kuwa watu wake.

158. U Mwendo Gani Nyumbani?
How Far From Home?

1. U mwendo gani nyumbani? Mlinzi akanijibu,
"Usiku sasa waisha,mahe kaibu."
Usihuzunike tena, bali ulemee mwendo
Hata ushike ufalme kule mwangani juu.

2. Na tena niliuliza, nchi yote ikajibu:
"Sasa mwendo watimika, milele karibu."
Usihuzunike tena, ishara kuu zasonga
Na viumbe vyangojea sauti ya Bwana.

3. Nikamwuliza shujaa, ndivyo kanitia moyo:
"Shikilia mapigano, kitambo yaisha."
Usihuzunike tena, kazi ifanye kwa moyo;
Tumeahidiwa tunu tuishapo shinda.

4. Siyo mbali na nyumbani! Fikara tamu njiani,
Latupoza roho, nalo lafuta machozi
Usihuzunike tena, kitambo tutakutana
Wenye furaha kamili nyumbani mwa Baba.









159. Anakuja Upesi
How Sweet are the Tidings

1. Anakuja upesi, Yesu Bwana wetu, Msafiri mbali na kwao;
Alisema dhahiri, "Nitakuja tena"; Amina; na uje, E Bwana.

Yuaja, Yesu atarudi sasa; Anakuja duniani.
Wasafiri wote watapumzika Yesu anaporudi tena.

2. Makaburi yote wafu wanapolala Yatafunguliwa tena;
Na mamilioni pale wataondoka tena, Wasione machozi kamwe.

3. Hatutatengana na hao tena huko; Nyimbo nzuri tutaimba.
Watakusanyika 'toka kila kabila, Miguuni pa Mwana-kondoo.

4. Aleluya Amin! Aleluya tena! Upendo wake unashinda!
Tutamsifu milele, hata tutashangaa, Jinsi alivyo tukomboa.

160. Watakatifu Kesheni
Watch, Ye Saints

1. Watakatifu kesheni, nguvu za mbingu zagonga;
Washeni taa tayari kwa kurudi kwake Bwana.

Yuaja, Yesu Mfalme, Yuaja myenye fahari,
Yesu yuaja enzini. Karibu Yesu, uje.

2. Piga mbiu, tangazeni habari ya ukombozi,
Ya mponya wa upendo nayo nguzu za samaha.

3. Falme nyingi zaangushwa, Panda ya saba hulia;
Tangaza neema yake kabla ya kupita saa.

4. Mataifa yapotea, nchi zajaa uchungu:
Kistro anaharakisha, Unabii unatimizwa.

5. Wenye dhambi njoni sasa, Kristo awapatanishe,
Mbio twaeni neema, kitambo muda waisha.

Nyimbo Za Kikristo: 121-140

121. Katika Wenye Dhambi
Chief Of Sinners

1.Katika wenye dhambi Ndimi mkuu wao—
Ila yesu akaja, Kwa dhanbi alikufa,
Akamimina damu Niupate uzima.

2.Ajabu pendo lake! Pendo lililo kuu,
Pendo lisilo mwisho, Lidumulo milele—
Lililonitafuta Inawa sikupenda.

3.Ingawa ni mbaya Kristo ni vyote kwangu;
Ajua haja zangu; Huzuni zangu, zake;
Hata katika vita, Akiwapo salama.
122. Yote Namtolea Yesu
All to Jesus I Surrender

1.Yote namtolea Yesu, moyo wangu ni wake:
Ninavutwa na upendo, kwa hivyo, najitoa.

Yote kwa yesu, Yote kwa Yesu,
Upendo wako hushinda; Yesu, natoa.

2. Yote namtolea Yesu, Nainamia pake;
Nimeacha na anasa, kwako Yesu nipokee.

3. Yote namtolea Yesu, Nifanye niwe wako;
Nipe Roho yako, Bwana, anilinde daima.

4. Yote namtolea Yesu, nami naona sasa,
Furaha ya ukombozi, nasifu jina lake.
123. Yesu Kwa Imani
My Faith Looks up to Thee

1.Yesu kwa imani, nakutumaini, peke yako;
Nisikie sasa, na kunitakasa, ni wako kabisa
Tangu leo.

2. Nipe nguvu pia za kusaidia moyo wangu;
Ulikufa wewe, wokovu nipewe, nakupenda wewe,
Bwana wangu.

3.Hapa nazunguka katika mashaka, na matata;
Palipo na giza utaniongoza, hivi nitaweza
kufuata.
124. Umechoka Umesumbuka
Are You Weary?

1. Umechoka, je, umesumbuka? mwambie Yesu sumbuko lako;
Unayalilia yapitayo? mwambie Yesu pekee.

Mwambie Yesu sumbuko lako, yu rafiki amini,
Hakuna rafiki kama yeye, mwambie Yesu pekee.

2. Je, machozi yakulengalenga? mwambie Yesu sumbuko lako;
Walemewa na dhambi rohoni? mwambie Yesu pekee.

3. Waogopa shida na majonzi? mwambie Yesu sumbuko lako;
Wasumbukia mambo yajayo? mwambie Yesu pekee.

4. Kuanzia kifo kukutisha? mwambie Yesu sumbuko lako;
Watamania ufalme wake? mwambie Yesu pekee.



125. Uniangalie
There's Life In A Look

1. 'Uniangalie' atwambia Yesu aliyetufia;
Msalabani ni uzima, Hapa utaipata hazina.

Kutazama Kalwari, Kutazama Kalwari,
Ni kupewa kuishi Kuutazama mti.

2. Ninapojaribiwa ghafla, Shetani hatanitenga;
Nikitazama msalaba Nguzu nitaipata kwa Bwana.

3. Msalaba nitautazama Kila wakati, daima.
Ahadi nitategemea, Hovi kabisa sitaangukaa.

126. Nina Haja Nawe
I Need Thee Every Hour

1. Nina haja nawe kila saa;
Hawezi mwingine kunifaa.

Yesu nakuhitaji vivyo kila saa!
Niwezeshe Mwokozi, nkujia.

2. Nina haja nawe; kaa nami,
Na maonjo haya, hayaumi.

3. Nina haja nawe; kila hali,
Maisha ni bure, uli mbali.

4. Nina haja nawe, Nifundishe,
Na ahadi zako zifikishe.

5. Nina haja nawe; mweza yote,
Ni wako kabisa siku zote.

127. Nisalama Rohoni Mwangu
When Peace Like A River

1. Nionapo amni kama shwari, au nionapo shida;
Kwa hali zote umenijulisha ni salama rohoni mwangu.

Salama rohoni,
Ni salama rohoni mwangu.

2. Ingawa Shetani atanitesa, nitajipa moyo kwani,
Kristo ameona unyonge mwangu; amekufa kwa roho yangu.

3. Dhambi zangu zote, wala si nusu, huwekwa msalabani;
Wala sichukui laana yake, ni salama rohoni mwangu.

4. Ee Bwana himiza siku ya kuja, panda itakapolia:
Utakaposhuka sitaogopa ni salama rohoni mwangu.

128. Taamini Nitii Pia
When We Walk with the Lord

1. Namwandama Bwana kwa aliloneno,
Njia zangu huning'azia;
Na nikimridhisha atanirudisha,
Taamini nitii pia.

Kuamini, Njia pweke ni hii
Ya furaha kwa Yesu: Amini ukatii.

2. Giza sina kwangu wala hata wingu,
Yeye mara huviondoa;
Oga, wasiwasi, sononeko, basi;
Huamini nitii pia.

3. Masumbuko yote, sikitiko lote;
Kwa mapenzi hunilipia;
Baa, dhara, dhiki, vivyo hubariki.
Taanimi nitii pia.

4. Mimi sitajua raha sawasawa
Ila yote Yesu kumtoa:
Napata fadhili na radhi kamili,
Taamani nitii pia.

5. Nitamfurahia na kumtumaini,
Majumbani na njia-njia;
Agizo natenda; nikitumwa hwenda,
Huamini, nitii pia.

129. Kumtegemea Mwokozi
'Tis So Sweet To Trust

1. Kumtegemea Mwokozi, kwangu tamu kabisa;
Kukubali neno lake nina raha moyoni.

Yesu, Yesu namwamini, nimemwona thabiti;
Yesu, Yesu yu thamani, ahadi zake kweli.

2. Kumtegemea Mwokozi, kwangu tamu kabisa
Kuamini damu yake nimeoshwa kamili.

3. Kumtegemea Mwokozi, kwangu tamu kabisa;
Kwake daima napata, uzima na amani.

4. Nafurahi kwa sababu nimekutegema;
Yesu, M-pendwa, Rafiki, uwe nami dawamu.

130. Yesu Kwetu Ni Rafiki
What A Friend We Have In Jesus

1. Yesu kwetu ni rafiki, hwambiwa haja pia;
Tukiombawka Babaye, maombi asikia;
Lakini twajikosesha, twajitweka vibaya;
Kama tulimwomba Mungu, dua atasikia.

2. Una dhiki na maonjo? Unamashaka pia?
Haifai kufa moyo, dua atasikia.
Hakuna mwingine Mwema, wa kutuhurumia:
Atujua tu dhaifu: Maombi asikia.

3. Je, hunayo hata nguvu, Huwezi kwendelea,
Ujapodharauliwa. ujaporushwa pia.
Watu wange kudharau, wapendao dunia.
Hukwambata mikononi, dua atasikia.

131. Baba Anilinda
I Trust In God

1. Namtegemea Mungu niwapo
Humo barani na baharini,
Yeye wa mbinguni anilinda.
Baba wa mbinguni anilinda.

Namwamini, Mungu anitunza (anitunza)
Milimani (milimani) au baharini (baharini) Baharini
Moyo Wangu (moyo wangu.) aulinda (aulinda).
Baba wa mbinguni anilinda.

2. La waridi alinawirisha,
Na huyo tai juu angani,
Nami kweli ananilinda,
Baba wa mbinguni anilinda.

3. Tunduni mwa simba namwamini,
Kwenye vita ama gerezani,
Motoni na furikoni,
Baba wa mbinguni anilinda.

4. Bondeni mwa giza na upweke,
Mchunga wangu yuanilinda,
Kwa upole aniongoza.
Baba wa mbinguni anilinda.

131a. Kwa Mahitaji Ya Kesho
Lord for Tommorrow and It's Needs

1. Kwa mahitaji ya kesho, Sian ombi;
Unilinde nisitende Dhambi leo;
Nisiseme neno baya, Mkombozi,
Nisifikiri uovu, leo hivi.

2. Ningefanya kazi sawa Na kuomba;
Ningekuwa mtu mwema Kila saa;
Mapenzi yako nifanye, Na kutii;
Nitoe mwili dhabihu, Leo hivi.

3. kama keo ningekufa Kwa ghafula,
Nitegemee ahadi Zako Bwana.
Kwa mahitaji ya kesho sina ombi;
Uniongoze, Nishike Leo hivi.

132. Bwana Ni Mchunga
The Lord is My Sherpherd

1. Bwana ni Mchunga, Sitahiji;
Majani mabichi mlisho yangu.
Ananinywesha maji Matulivu;
Atanirudisha nikipotea.

2. Nipitapo bondeni mwa mauti
U mlinzi wangu—sitaogopa;
Fimbo lako latoshakunilinda;
Ukinifariji sina hasara.

3. Kati ya mateso mea waandaa,
Na kikombe changu kinafurika;
Umenipaka kichwani mafuta;
Nitaulizaje zaidi kwako?

4. Wema na fadhili zinifuate
Siku zangu zote hata milele;
Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana
Katika ufalme wa pendo lake.




133. Po Pote Na Yesu
Anywhere With Jesus

1. Po Pote na Yesu nina furaha; Anitumako Yesu ndiyo raha.
Asipokuwako hapanifai, Akiwapo Yesu, mimi sitishwi.

Po pote, po pote, sina mashaka:
Po pote na Yesu naweza kwenda.

2. Akiwapo yesu, si peke yangu; Na nijapotupwa, akali wangu;
Ajaponiongoza njia nbaya, Niwapo na Yesu nashukuria.

3. Akiwapo yesu naweza lala, naweza pumzika hata kiyama;
Kisha nitakwenda kwake milele, akiwapo Yesu furaha tele.
134. Tafuta Daima Utakatifu
Take Time to be Holy

1. Tafuta daima utakatifu;
Fanya urafiki na wakristo tu;
Nena siku zote na Bwana wako,
Baraka uombe kwa kila jambo.

2. Tafuta saima utakatifu:
Uwe peke yako ukimwabudu;
Ukimwangalia Mwokozi wako,
Utabadilishwa kama alivyo.

3. Tafuta daima utakatifu;
Kiongozi wako awe Yesu tu;
Katika furaha au huzuni
Dumu kumfuata Yesu Mwokozi.

4. Tafuta daima utakatifu;
Umtawaze Roho moyoni mwako,
Akikuongoza katika haki,
Hufanywa tayari kwa kazi yake.



135. Kwa Maombi Nachangamka
Sweet Hour Of Prayer

1. Saa heri ya maombi, sasa kwako tunarudi,
Sumbuku ya kuondoa, shida zitu na pungufu.
Taabuni mara nyingi, roho zetu zimepona,
Mashakani tumeshinda, wakati wa saa tamu.

2. Saa heri ya maombi, Twapelika dhiki zetu
Kwake aliyeahidi kubariki wenye haja.
Huagiza tumwendee, tutegemee neno lake,
Hivyo tumwekee yote, wakati wa saa tamu.

3. Saa heri ya maombi, tutazidi kuingia
Bomani mwetu na ngome, hata tuishapo mwendo.
Yesu atatusikea, tutamtafuta daima,
Na tutakapolutana tutamwona—saa tamu!


136. Niwe Kama Yesu
Teach Me Father

1. Unifundishe, Baba; Ile njia ya sala;
Uniendeshe sana, Niwe kama Yesu.

Niwe kama Yesu, Niwe kama Yesu,
Uniongoze, Baba; Niwe kama Yesu.

2. Unipe pendo, Baba, Watu kuwaokoa;
Nyumbani na mjini. Niwe kama Yesu.

3. Na unifahamishe, Wakati ndio mfupi;
Unibidishe, bwana, Niwe kama Yesu.
137. Saa Heri Ya Sala
'Tis the Blessed Hour of Prayer

1. Saa heri ya sala tunapojidhili,
Kama tukija kwake yesu rafiki.
Tukiwa na imani kwamba yu mlinzi,
Waliochoka sana watapata raha.

Saa ya sala, iliyo heri;
Waliochoka sana watapata raha.

2. Saa heri ya sala, ajapo mwokozi,
Ili awasikie watoto wake.
Hutwambia tuweke miguuni pake
Mizigo yetu yote: tutapata raha.

3. Saa heri ya sala, wawezapo kuja
Kwa Bwana Yesu wanaojaribiwa;
Moyo wake mpole, atawarehemu;
Waliochoka sana watapata raha.

4. Saa heri ya sala tutakapopewa
Mibaraka ya roho, tukimwamini;
Kwa kuamini kweli hatutaogopa;
Waliochoka sana watapata raha.

138. Nitakuandama Kote
I Will Follow Thee

1. Nitakuandama kote, nitakapoagizwa,
Wewe ukiniongoza nami nitaandama.

Nitakuandama Kote, naam, ulinifia;
Kwa neema yako Bwana napenda kuandama.

2. Njia ijapoparuza kwa miiba na fujo,
Ulitangulia Mbele nami nitaandama.

3. Nijapokuta taabu na majaribu kote,
Nakumbuka shida yako, nami nitaandama.

4. Nijapoona ukiwa na mateso makali,
Wewe uliyatikiza nami nitaandama.

5. ijapo wanipeleka vilindini mwa giza,
Wewe uliyatikiza nami nitaandana.

139. Uliniimbie Tena
Sing them over again

1. Uliniimbie tena, Neno la uzima;
Uzuri wake nione, Neno la uzima;
Neno hili zuri, lafundisha kweli:

Maneno ya uzima ni maneno mazuri,
Manemo ya uzima ni naneno mazuri.

2. Kristo anatupa sote, Neno la uzima:
Mwenye dhambi asikie Neno la uzima:
Latolewa bure, Tupate wokovu:

3. Neno tamu la Injili, neno la uzima;
Mwenye dhambi asikie Neno la uzima:
Litatutakasa, kwa haki ya Mwana:

140. Hivi Nilivyo Unitwae
Just as I am

1. Nitwae hivi nilivyo, umemwaga damu yako,
Nawe ulinyoniita, Bwana Yesu, sasa naja.

2. Hivi nilinyo; si langu kujiosha roho yangu;
Nisamehe dhambi zangu, Bwana Yesu, sasa naja.

3. Hivi nilivyo; sioni kamwe furaha moyoni,
Daima ni mashakani, Bwana Yesu, sasa naja.

4. Hivi nilivyo kipofu, maskini na mpungufu;
Wewe ndiwe u tajiri, Bwana Yesu, sasa naja.

5. Hivi nilivyo, mimi tu, siwezi kujiokoa;
Na wewe hutanikataa, Bwana Yesu, sasa naja.

6. Hivi nilivyo; mapenzi yamenipa njia wazi;
Hali na mali sisazi, Bwana Yesu, sasa naja.

Nyimbo Za Kikristo: 101-120

101. Yesu Akwita
Jesus Is Tenderly Calling Today

1. Yesu akwita, akwita wewe, Uje leo, uje leo,
Kwani kusita, akwita wewe Unatanga upeo;

Msikie, msikie,
Yesu akwita, ujitoe moyo sasa.

2. Wliochoka, na wapumzike, Uje leo, uje leo,
Wenye mizigo, wenye huzuni Wapate mapumziko.

3. Anakungoja uliye yote, Uje leo, Uje leo,
Uliyekosa, usijifiche: Woshwe, uvikwe nguo.

4. Yesu asihi wakawiao, Waje leo, waje leo,
Watafurahi waaminio; Amka, upesi, Njoo.

102. Mlango Pa Moyo
There's a Stranger as the Door

1. Mlangoni pa moyo; Mgeni! (Amesimama)
Amesimama pale, Mgeni! (Amesimama)
Umkaribishe sasa,
Umkaribishe Mwana
Wa Baba wa upendo: Mgeni! (Umkaribishe)

2. Moyo wako kwa Bwana, Fungua. (Fungulieni)
Asikuache mbali, Fungua. (Fungulieni)
Umkubali Rafiki,
Roho atafariji
Naye atakutunza: Fungua. (Fungukieni)

3. Usikie sauti Ya Bwana. (Uisikie)
Uyachague mambo Ya Bwana. (Mambo ya Bwana)
Ufungue mlango,
Usimwambie bado:
Jina lake tumai---- Yu Bwana. (Jina la Bwana)

4. Na ufungue moyo, Kwa Bwana (Fungulieni)
Utapewa msaada, Wa Bwana (Msaada wetu)
Uzuri utavikwa
Dhambi ataondoa,
Ukifungua moyo. Kwa Bwana (Fungulieni)





103. Njoni Kwangu
Softly and Tenderly

1. Yesu huita kwa upole mwingi, atwita wewe nami;
Moyoni mwetu hungoja, hukesha, Hukungojea wewe.

"Njoni kwangu, Mliochoka, njoni:
Yesu huita kwa upole mwingi, Akwita, "uje kwangu"

2. Atuombeapo usikawie, Hutuombea sisi;
Usidharau wema ma huruma, Huruma kwetu sisi.

3. Siku za maisha hupota hima, Hupita kwako, kwangu;
Usiku waja, kifo kinakuja, Huja kwako na kwangu.

4. Fikiri juu ya upendo wake, Upendo kwako, kwangu;
Dhambi zetu amekwisha samehe. Masamaha ni yetu.














104. Yesu Aliniita "Njoo"
I Heard the Voice of Jesus Say

1. Yesu aliniita, "Njoo Raha iko kwangu,
Kichwha chko ukilaze Kifuani mwangu"
Nilikwenda kwake mara, sana nilichoka;
Nikapata kwake raha Na furaha tena.

2. Yesu aliniita, "Njoo, Kwangu kuna maji;
Maji ya Uzima, bure, Unywe uwe hai."
Nilikwenda kwake mara na maji nikanywa;
Naishi kwake na kiu Kamwe sina tena.

3. Yesu aliniita, "Njoo, Dunia i giza,
Ukinitazama, nuru Takung'arizia.'
Nili kwenda kwake mara, Yeye jua langu,
Ni kila wakati mwanga Safarini Mwangu.














105. Mchungaji Mpenzi
Lovingly, Tenderly Calling

1. Mchungaji mpenzi hukuita uje
Katika zizi lake Panapo salama;
Akina wanawake, waume vijana,
Yesu aliye kweli, huwaita kwake

Huita kwa moyo wa huruma, 'Uluyepotea uje kwangu';
Hivi kukungoja anadumu Bwana Yesu Mchunga.

2. Akatoa maisha kwa ajili yetu;
Ataka wapotevu waje kwake sasa;
Tusijihatirishe; Kwake tu salama;
Sikia wito wake, Mchungaji wetu.

3. Tusikawie tena, adui shetani,
Kama Mbwa wa mwitu, atatuharibu;
Tunaitwa na Yesu, Mkombozi wetu,
Tuingie zizini, panapo nafasi.











106. Huna Kitu Kwa Yesu?
Nothing for Jesus

1. Ukitafuta mali, Huna wasaa kwa Yesu?
Kwa matendo ya haki Huna wasaa kwa Yesu?
Ansa za kunia, Mambo yako ya raha
Haya unatafuta; Huna wasaa kwa yesu?

2. Mambo yanakusonga: Kwake huna nafasi?
Watekwa na dunia, Kwake huna nafasi?
Humwani m-langoni, Anapopiga hodi?
Daima hukusihi: Kwake huna nafasi?

3. Sa-a ni za thamani, Kwake huna nafasi?
Wala hamfnyi bidii, Kwake hamnayo kazi?
Hamkufika kwao Waliomo shimoni
Na waliopotea? Kwake hamnayo kazi?

4. Na wazaa majani tu? Huna tunda kwa Yesu?
Mikono i mitupu, Huna tunda kwa Yesu?
Huna chembe kwa ghala kazi yako kulipa;
Wala huna furaha Unapomwona Yesu?










107. Nipo Bwana, Nitume
Hark! The Voice Of Jesus

1. Sauti ni yake Bwana, "Kwenda, nani tayari"
Mavuno yanakawia, Nani atayavuna?
Kwa kudumu amaita, Zawadi atatoa;
Nani atakayejibu "Nipo Bwana, nitume."

2. Kana huwezi safari Hata Nchi za mbali,
Pana watu karibuni Wasio mjua Yesu;
Kama huwezi kusema Jinsi ya malaika,
Waweza kuutangaza Upendo wa mwokozi.

3. Ingawa huwezi kuwa Mkesha mlangoni,
Ukiwatolea watu Nafasi ya uzima;
Kwa sala na kwa sadaka Watoa msaada,
Kama Harun mwaminifu, Kuinua Mikono.

4. Roho za watu zikifa, Bwana akikuita,
Usiseme kwa uvivu, "Hakuna kazi kwangu."
Kwa furaha anza kazi Ile akiyokupa,
Ukajibu mara moja "nipo Bwana, nitume."









108. Tumesikia Mbiu
We Have Heard a Joyful Sound


1. Tumesikia mbiu: Yesu huokoa;
Utangazeni kote, Yesu Huokoa.
Tiini amri hiyo: nchimi baharini,
Enezeni mbiu hii: Yesu huokoa.

2. Imba nawe askari: Yesu huokoa;
Kwa nguvu ya kombozi, Yesu huokoa;
Imbeni wenye shida, unapounwa moyo,
Na kaburini imba: Yesu huokoa.

3. Mawimbini uenee. Yesu huokoa.
Wenye dhambi jueni: Yesu huokoa;
Visiwa na viimbe, vilindi itikeni,
Na nchi shangilie: Yesu huokoa.

4. Upepo utangaze: Yesu huokoa.
Mataifa ya shangaa: Yesu huokoa;
Milimani, bondeni, sauti isikike
Ya winbo wa washindi: Yesu huokoa.








109. Anisikiaye
Whoever heareth

1. Anisikiaye, aliye yote, sana litangae, wajue wote,
Duniani kote neno wapate, atakye na aje!

Ni "atakaye," Ni "atakaye";
Pwani hata bara, na litangae:
Ni Baba mpenzi alinganaye atakaye na aje.

2. Anijiliaye, Yesu asema, asikawe, aje hima mapema
Ndimi Njia, kweli, ndimi uzima: atakaye na aje!

3. Atakaye aje, ndiyo ahadi; atakaye hiyo haitarudi!
Atakaye lake, ni la ahadi! Atakaye na aje.

110. Mlango Wazi
There is a Gate

1. Mlango uko wa wema, Mlango wazi huo:
Yesu aneufungua Na hakuna kufunga.

Mlango wazi, ajabu, Uliachwa wazi kwangu?
Kwangu, Kwangu? Wazi, wazi kwangu?

2. Mlango hukaa wazi watu waokolewe:
Maskini ma matajiri Wa mataifa yote.

3. Maadanu mlango wazi, Rafiki kaza mwendo;
Msalaba ukubali- Amana ya upendo.

4. Msalaba tutabeba Daima, na furaha!
'pendo la Yesu hushinda. Unainama kwake!















111. Tabibu Mkuu
The Great Physician

1. Tabibu mku-u huyu, Yesu mwenye huruma:
Atuletaye faraja : Yesu mwokozi wetu.

Imbeni, Malaika Sifa za bwana wetu;
Jina la pekee kwetu, ni la Yesu Bwana.

2. Mwana kondo-o msifuni Mwokozi:
Hatia zote na dhambi Huziondoa Yesu.

3. Hakuna jina jingine Linalofa-a sifa:
A-u kutufurahisha, Isipo kuwa lake.

4. Naye atakapokuja Na utukufu wake,
Tutafurahi milele kuka-a kwake Bwana.


112. Wewe Umechoka Sana?

1. Wewe umechoka sana? Wataka raha?
Kwake Yesu utapata –Msaada.

2. Alama anazo Yeye? Sana! Makovu
Ya mikono, na miguu, Na mbavu.

3. Naye amevikwa taji Kichwani mwake?
Taji, kweli, alivikwa –Miiba!

4. Huku nikimfuata, Nipate nini?
Maonjo nje, na ndani—Amani.

5. Kwamba namwandama Yeye, Mwisho ni nini?
Kurithi futaha naye---Milele.

113. Bubujiko
There Is a Fountain

1. Damu imebubujika, Ni ya Imanweli,
Wakioga wenye taka, Husafiwa kweli.

2. Ilimpa kushukuru Mwivi mautini;
Nami nisiye udhuru, Yanisafi ndani.

3. Kondo-o wa kuuawa, Damu ina nguvu,
Wako wote kuokoa kwa utimilivu.

4. Bwana, tangu damu yako Kunisafi kale,
Nimeimba sifa zako. 'taimba milele.

5. Bwana, umenikirimu Nisiyestahili
Kwa damu yako, sehemu Ya mali ya kweli.

6. Nikubali kumwimbia Mbinguni milele.
Mungu nitamsifia Jina lako pweke.

114. Yesu Nataka Kutakaswa Sana
Lord Jesus, I Long to be Perfectly Whole

1.Yesu Mwokozi Ili nitakaswe, nataka mouo uwe enzi Yako.
Ukiagnushe kilichoinuka unioshe sasa niwe mweupe.

Mweupe tu, ndiyo mweupe,
Ukiniosha nitakuwa safi.

2. Bwana Yesu sasa unitazame, unifanye niwe dhabihu hai."
Najitoa kwako, na moyo, vyote; unioshe sana niwe mweupe.

3.Bwana kwa hiyo nakuomba sana, nakuongojea miguuni pako,
Wanaokuja hutupi kamwe, unioshe sasa niwe mweupe.

115. Naendea Msalaba
I am Coming To The Cross

1. Naendea msalaba, Ni mnyonge, mpofu,
Yapitayo naacha nipe msalaba tu.

Nakutumaini tu, wee Mwana wa Mungu;
Nainamia kwako; Niponye sasa, Bwana.

1. Nakulilia sana: Nalemewa na dhambi;
Pole Yesu asema: "Nitazifuta zote."

3. Natoa vyote kwako, nafasi nazo nguvu,
Roho yangu na mwili viwe vyako milele.

4. Kwa damu yake sasa amenivuta sana,
Upendo hubidisha, nimtafute Mwokozi.
116. Moyo Safi
One Thing I of the Lord Desire

1. Bwana ninataka hili, kwa kuwa nimechafuka,
Kwa moto au kwa maji unisafishe kabisa.

Unisafishe Mwokozi ndani, na nje, kwa moto—
Utakavyo: ili dhambi ife kwangu, ife kwangu.

2. Kupewa hekima yote, itakuwa tunu kubwa;
Lakini moyo safi ni, bora kwangu, bora kwangu!

3. Mpaka moyo ni safi siwezi kuyafahamu
Mambo mazuri ya mbingu, mambo mazuri ya mbingu.

117. Wamwendea Yesu
Have You Been to Jesus?

1.Wamwendea Yesu kwa kusafiwa. Kuoshwa kwa damu ya kondoo?
Je, neema yake yatumwagiwa? Waoshwa kwa damu ya Kondoo?

Kuoshwa, kwa damu Itutakasayo ya Kondoo?
Ziwe safi nguo nyeupe sana; waoshwa kwa damu ya Kondoo.

2.Wamwandana daima Mkombozi.Waoshwa kwa damu ya Kondoo?
Yako kwa Msulubiwa mavazi? Waoshwa kwa. Damu ya Kondoo?

3.Atakapokuja Bwana-arusi Uwe safi katika damu!
Yafae kwenda Mbinguni mavazi: Yaoshwa kwa damu ya kondoo?

4.Yatupwe Yalipo na takataka; Uoshawe kwa damu ya Kondoo:
Huoni kijito chatiririka Uoshwe kwa damu ya Kondoo?


118. Nilipotoka Kabisa
I've Wandered Far Away

1.Nilipotoka kabisa, sasa narudi
Nikakawia dhambini, Bwana narudi.

Narudi nyumbani: daima kwako.
Kwa upendo nipokee: Naja nyumbani.

2.Nikasusurika sana, sasa narudi
Mwenye uchungu natubu, Bwana narudi.

3.Nimechoka maovuni, sasa narudi;
Pendo lako lanivuta, Bwana narudi.

4. Ndilo tumaini langu, sasa narudi;
Yesu alinifilia, Bwana narudi.

5. Damu yake yanitosha, sasa narudi;
Unioshe kenyekenye, bwana narudi.

119. Alilipa Bei
I Hear the saviour Say

1.Yesu anasema, "Wewe huna nguvu
Kesha ukaombe, Na uje, Mwanangu.

Alilipa bei, Nawiwa naye;
Dhambi ilitia waa, aliiondoa.

2. Bwana, nimeona Uwezo wako tu
Waweza 'takasa Mioyo michafu.

3. Sina kitu chema Kudai Neema,
Hivi nitafua Mavazi kwa damu.

4. Ninaposimama Juu ya mawingu,
Taji nitaweka Miguuni pa Yesu.


120. Msalaba wa Yesu
Jesus, Keep Me Near The Cross

1. Msalaba wa Yesu, Nikae karibu;
Pale pana chemchemi Ya kuponya dhambi.

Pale msalaba Msalaba wake,
Huo ni sifa yangu Kwa maisha yote.

2. karibu msalaba Nalitetemeka,
Pendo likaniona Likanirenemu.

3. Unikumbushe yesu, Nikuone pale;
Niupate upendo Na kuvutwa nao.

4. Karibu msalaba, Kwa kutegimea,
Kukesha na kungoja, Nitakaa pale.

Nyimbo Za Kikristo: 91-100

91. Kaa Nami
Abide with Me

1. Kaa nami, ni isiku tena;
Isiniache gizani, Bwana.
Msaada wako haukomi;
Nili peke yangu, kaa nami.

2. Siku zetu hazakawi kwisha;
Sioni la kunifurahisha;
Hakuna ambacho kakikomi,
Isiye na mwisho kaa nami.

3. Nina haja nawe kila saa;
Sina mwingine wa kunifaa
Mimi nitaongozwa na nani
Ila wewe? Bwana, kaa nami.

4. Sichi neno uwapo karibu;
Nipatalo lote si taabu;
Kifo na kaburi haviumi;
Nitashinda kwako, kaa nami.

5. Nilalapo nikuone wewe,
Gizani mote nimulikiwe;
Nuru za mbinguni hazikomi,
Siku zangu zote; kaa nami.

92. Magharibi Jua
Day is Dyding in the West

1. Magharibi jua limekwisha kushuka,
Mwezi na nyota sasa vinamsifu Muumba wa usiku.

Mungu Mtukufu, Mungu Mkuu,
Wote juu mbinguni, na wanadamu chini Twakusifu.

2. Mpaji wa uhai, ukaaye mbinguni.
Utuhifadhi sisi, tufahamu gizani, U karibu.

3. Mapenzi yako makuu yawe nasi usiku,
Tuli usingizini, kucha vivyo roho Tushukuru.

4. Na utakapo kuja na nguvu kutawala,
Mungu wangu kubali kunichikua mimi Uliko juu.

Baba, Mwana, Roho, Mungu wetu,
Wote juu mbinguni, na wanadamu chini Twakusifu.

93. Jua La Rohoni Mwangu
Sun of My Soul

1. Jua la rohoni mwangu, mpendwa Mwokozi wangu;
Usiku giza hapana, ukiwa karibu Bwana.

2. Nikipata usingizi, nijaze fikara hizi,
Ni tamu sana, nilale pendoni mwako milele.

3. Kaa nami, ewe Bwana, Usiku kama mchana,
Nisiishi mbali nawe; ni uhai kuwa nawe.

4. Kama mtoto mnyonge ameshawisha atange,
Mtafute Ewe Bwana, ujirudishie tena.

5. Wagonjwa wape amani, waneemeshe maskini,
Walio, Mtulizi, wape wote usingizi.

6. Asubuhi tutokapo, tukaribishe tulipo;
Twingiapo duniani tuwe mwako mkononi.

94. Po Pote Mashamba Yajaa
Far And Near The Fields

1. Po pote mashamba yajaa, tele nafaka pevu,
Po pote yang'aa meupe bondeni na nyandani.

Mwenye mavuno, twasihi upeleke wavuni,
Wayakusanye mazao, hata kazi yaishe.

2. Wapeleke uchaoni, waende na jotoni,
Hata jua lishukapo wakusanye ko kote.

3. Enyi wakazi wa Bwana yaleteni mazao,
Na jioni ingieni kwake na furaha kuu.

95. Zileteni Zaka Kwa Hazina
Bring Ye All The Tithes

1. Sikieni neno la Mungu Wetu, Zileteni zaka kwa hazina
Leteni na mioyo yenu yote; mibaraka itakuja.

Zileteni zaka kwa hazina, kanijaribu sasa nazo;
Nitakupeni mibaraka, zaidi ya nafsi ya kupewa.

2. Wataka Roho Mtakatifu kwako? Uzilete zaka kwa hazina
Ukae karibu na Bwana wako, ndipo utakapo barikiwa.

3. Je! Unakasoro na Bwana wako? Uzilete zaka kwa hazina
Uzilete kama alivyosema, Ndipo utakapo barikiwa.

4. Ushukuru Bwana na moyo wote, unapoleta zaka ghalani;
Usadiki ahadi zake zote, ndipo utakapo barikiwa.

5. Tuimbe sote nyimbo za furaha, tunapoleta zaka ghalani
Twimbe kabisa na furaha kubwa, kwani tutabarikiwa.

96. Mali Yako Sasa
We Give Thee But Thine Own

1. Mali yako sasa, Bwana, tutatoa;
Hatuna yaliyo yetu, Yote ni vipaji.

2. Sisi watumishi, Twaungama deni;
Tunge irudisha kwake, Iliyo ya Bwana.

3. Utusaidie, Upendo kujua,
Kwa ajili yao wote Walio gizani.

4. Neno tumaini na kutegemea:
Kwamba lote tufanyalo, Tulifanye kwako.

97. Sioshwi Dhambi Zangu
What Can Wash Away My Sin?

1. Sioshwi dhambi zangu bila damu yake Yesu,
Hapendezewi Mungu bila damu yake Yesu.

Hakuna kabisa dawa ya makosa
Ya Kututukasa ila damu yake Yesu.

2. La kunisafi sina ila damu yake Yesu,
Wala udhuru tena ila damu yake Yesu.

3. Sipati patanishwa bila damu yake Yesu,
Hukumu yanitisha, bila damu yake Yesu.

4. Sipati tumaini bila damu yake Yesu,
Wema wala amani bila damu yake Yesu.

5. Yashinda ulimwengu, iyo damu yake Yesu,
Na kutufikisha juu, iyo, damu yake Yesu.

98. Nilikupa Wewe
I Gave My Life For Thee

1. Nilikupa wewe, damu ya moyoni,
Ili wokolewe, winuke ufuni.

Nimekunyima ni wewe? Umenipa nini?
Nimekunyima ni wewe? Umenipa nini?

2. Nilikupa myaka yangu duniani;
Upate inuka, kuishi mbinguni.

3. Nimekuletea, huku duniani;
Pendo na wokovu, zatoka mbinguni.

4. Nipe siku zako, Udumu mwangani;
Na taabu yako, wingie rahani.

Nafsi, nafsi, pendo, mali, twae Imanueli.
Nafsi, nafsi, pendo, mali, twae Imanueli.











99. Twende kwa yesu
Come To the Saviour, Make No Delay

1. Twende kwa Yesu mimi nawe, njia atuonya tuijue,
Imo chuoni; na mwenyewe, hapa asema njoo!

Na furaha tutaiona, myoyo iki takasa sana;
Kwako mwokozi, kuonana, na milele kukaa.

2. "Wana na waje," atwambia furahini kwa kusikia;
Ndiye Mwokozi wetu hasa, na tumtii, njoni.

3. Wangojeani? Leo yupo: sakiza sana asemapo;
Huruma zake zitwitapo, ewe kijana, njoo.

100. Kuwatafuta
Seeking The Lost

1. Kuwatafuta wasioweza, kuomba wamrejee Yesu,
Kuwaambia maneno yake "Njooni kwangu, nawapenda."

Nitakwenda (Nitakwenda) niwatafute wapotevu (Wapotevu) wageuke,
Waingie (Waingie) katika zizi la Mwokozi (la mwokozi) Yesu Kristo.

2. Kuwatafuta wasioweza, waonyeshwe Mwokozi wetu,
Kuwaongoza, wapate wote uzima ule milele.

3. Kazi hiyo nataka kufanya, leo nimesikia mwito
Kuwainua waangukao, waletwe kwake Yesu Njia.

Nyimbo Za Kikristo: 81-90

81. Siku Sita Zimepita
Another Six Days' Work

1. Siku sita zime pita, Sabato tena karudi;
Shangilie roho yangu, itukuze kwa busara.

2. Msifuni awapaye pumziko tamu wachovu,
Kwake roho yatulizwa, kupita siku nyingine.

3. Moyo wetu ufurahi, na kutoa mashukuru;
Ujalizwe raha ile, yasipitikwa kamwe.

4. Raha hiyo ya rohoni, ni amana ya pumziko
Ambalo limewekwa juu, kikomo cha masumbuko.

82. Ni Siku Ya Furaha
O Day Of Rest

1. Ni siku ya furaha, ni siku ya nuru;
Nasi twaona raha, Kuja kushukuru;
Leo watu wa Mungu, wadogo, wakubwa,
Hukaribia mbingu, lilipo baraka.

2. Leo, ndiyo bandari, nasi twawasili,
Hiyo bustani nzuri, ya nyingi fadhili:
Kijito cha baridi kimefanya ziwa,
Na kiu ikizidi, twanywa maridhawa.

3. Leo ngazi na iwe ifakayo juu,
Mawazo na yasiwe ya duniani tu;
Leo ni kujilisha chakula cha mbingu,
Na kujifurahisha kwa mambo ya Mungu.

83. Ewe Skuli Ya Sabato
Sweet Sabbath School

1. Ewe skuli ya Sabato,
U pazuri sana;
Moyo wangu wanivuta,
Nije kwako leo.

Sabato . . . ni nzuri . . .
Sabato . . . ni nzuri . . .
Moyo wangu wanivuta,
Nije kwako leo.

2. Moyo wangu mpotovu,
Hapa una raha;
Ndipo nimwonapo Yesu,
Nije kwako leo.

3. Hapa Yesu mwenye pendo
Aniita pole:
Nimtolee moyo Yeye,
Nije kwako leo.

84. Ikumbuke Sabato
Don't Forget the Sabbath

1. Ikumbuke kote Sabato ya Bwana,
Siku tamu na bora, kupita nyingine;
Yatuletea raha, na furaha kweli,
Mwanga wake hungaza, urembo wa Yesu.

Karibie, karibie, Sabato tamu;
Karibie, Yesu pia, Bwana wa raha.

2. Itakase kweli, ukamsifu leo,
Yeye aliye sema "Mimi ndiye njia";
Nasi tukimfuata mkombozi hapa.
Atatunywesha tele maji ya uzima.

3. Siku ya nderemo! Tupishe wakati,
Tukimwimbia Yesu Rafiki Mpendwa;
Mponya wetu leo, U mwema ajabu!
Ukae kwetu, Bwana, moyoni daima.

85. Salama Tumepita
Safely Through Another Week

1. Salama tumepita, safarini juma hii,
Tumwendee Mwokozi, atubariki sasa:
Siku hiyo ya raha, siku bora ya juma;
Siku hiyo ya raha, siku bora ya juma.

2. Utupe nuru leo toka hazina yako;
Ondoa dhambi zetu, tupokee na pendo;
Mikono yapumzika, tuishi ndani yako,
Mikono yapumzika, tuishi ndani yako.

3. Twakusanyika hapa, tusifu jina lako;
Ukaribie kwetu, tupe neema Bwana;
Utamu tusikize, wa raha ya milele:
Utamu tusikize, wa raha ya milele:

4. Injili yako leo, ishike wenye dhambi;
Itupe nguvu nyingi, iponye wenye shida;
Mioyo yetu shangaza, vyakula utulishe,
Mioyo yetu shangaza, vyakula utulishe.

86. Ukaribie Tena
Welcome, Welcome, Day of Rest

1. Ukaribie tena, ewe siku ya raha;
Roho yakusalimu kama mwanga wa mbingu.

2. Raha yako tulivu, yafurahisha moyo;
Yatuliza taabu, hata waisha mwendo.

3. Ee siku takatifu, sifa na maombi,
Na kutuhekimisha., baraka yako kubwa.

87. Siku Ya Sabato
Thy Holy Sabbath Lord

1. Siku ya Sabato, siku takatifu,
Watu wako Mungu wetu, waipenda sana.

2. Ulitakasa, uliibariki,
Siku hiyo ya Sabato, siku yako Bwana.

3. Nasi tubariki tukikuabudu,
Katika siku ya raha, siku yako Bwana.

4. Halafu mbinguni, pamoja na Wewe.
Tunataka kuzishika Sabato za Bwana.

88. Siku Hii Ya Sabato
How Sweet Upon This Sacred Day

1. Siku hii ya Sabato, Tamu kufikiri
Juu ya Mungu na Mbingu Kuacha dunia.

2. Tamu kusikia Neno Toka mhubiri
Anayefundisha toba, Tupate uzima.

3. Katika vita na dhambi, Ikiwa twashindwa,
Yeye atatupa nguvu Aonaye moyo.



















89. Asubuhi
Lord, In The Morning

1. Bwana asubuhi kucha nitakuinua
Sauti yangu kuomba, nipate baraka.

2. Nakuomba roho yako niongozwe nayo;
Nifanye yanipasayo, na mapenzi yako.

3. Wanaokutegemea, U Mlinzi wao;
Matumaini wanayo, utayatimiza.

4. Na kwa wingi wa fadhili, Nyumbani mwako juu
Nitaingia na wimbo, Pale kusujudu.

90. Mapya Ni Mapenzi
New Every Morning

1. Mapya ni mapenzi hayo, Asubuhi tuonayo;
Saa za giza hulindwa, Kwa uzima kuamka.

2. Kila saku, mapya pia, Rehema, wema na afya,
Wokovu na msamaha, Mawazo mema, furaha.

3. Tukijitahidi leo Na mwendo utupasao,
Mungu atatueleza Yatakayompendeza.

4. Mamboyetu ya dunia Bwana atayang'aria,
Matata atageuza Yawe kwetu ya baraka.

5. Yaliyo madogo, haya Bwana tukimfanyia,
Yatosha: tutafaidi Huvuta kwake zaidi.

6. Ewe Bwana, siku zote, Tusaidie kwa yote:
Mwendo wetu wote vivyo, Uwe kama tuombavyo.